Wastara atoka kivingine, afungua milango mipya

Wastara atoka kivingine, afungua milango mipya

matumbo

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
7,224
Reaction score
3,951
28-635x336.jpg


KATIKA kujiongezea vyanzo vya mapato, staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ameamua kujizatiti zaidi kwenye biashara ambapo sasa amefungua sehemu ya kuoshea magari maarufu kama Car Wash iliyopo Tabata, Dar es Salaam.Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma akiosha moja ya gari lililofika kupata huduma ya uoshaji katika ‘Car Wash service station’ yake iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam.Akizungumza katika uzinduzi wa car wash hiyo aliyoipa jina la Mamii Car Wash, Wastara alisema ameamua kujiimarisha zaidi kibiashara kwa kuwa soko la filamu kwa sasa lipo chini na lina mikikimikiki mingi.
33.jpg

Huu ni mwonekano wa kituo cha Wastara cha kuoshea magari.
“Hakuna cha maana ninachopata kwenye filamu zaidi ya umaarufu tu. Wakati marehemu mume wangu (Sajuki) alipokuwa hai alikuwa anakimbizana kuhakikisha mambo yanakwenda sawa lakini mimi kama mtoto wa kike, nashindwa kufuatilia vizuri.“Kwa sasa nimeamua kujikita zaidi kwenye biashara, filamu nitafanya lakini mara chache. Hapa nasubiri Ramadhani ianze na ipite, natarajia kufungua na hoteli hapahapa baada ya mfungo,” alisema Wastara.
 
Where there is a will, there is a way
 
big up mama, keep on going i adore u much
28-635x336.jpg


KATIKA kujiongezea vyanzo vya mapato, staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma ameamua kujizatiti zaidi kwenye biashara ambapo sasa amefungua sehemu ya kuoshea magari maarufu kama Car Wash iliyopo Tabata, Dar es Salaam.Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma akiosha moja ya gari lililofika kupata huduma ya uoshaji katika ‘Car Wash service station' yake iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam.Akizungumza katika uzinduzi wa car wash hiyo aliyoipa jina la Mamii Car Wash, Wastara alisema ameamua kujiimarisha zaidi kibiashara kwa kuwa soko la filamu kwa sasa lipo chini na lina mikikimikiki mingi.
33.jpg

Huu ni mwonekano wa kituo cha Wastara cha kuoshea magari.
"Hakuna cha maana ninachopata kwenye filamu zaidi ya umaarufu tu. Wakati marehemu mume wangu (Sajuki) alipokuwa hai alikuwa anakimbizana kuhakikisha mambo yanakwenda sawa lakini mimi kama mtoto wa kike, nashindwa kufuatilia vizuri."Kwa sasa nimeamua kujikita zaidi kwenye biashara, filamu nitafanya lakini mara chache. Hapa nasubiri Ramadhani ianze na ipite, natarajia kufungua na hoteli hapahapa baada ya mfungo," alisema Wastara.
[/QUOTE]
 
Acha utani...kila mtu siku hizi anafungua car wash...ubunifu gani upo hapo!?
 
Acha utani...kila mtu siku hizi anafungua car wash...ubunifu gani upo hapo!?

Mwingine nani, labda bongo kuna vumbi sana magari yanabuka mara kwa mara.
 
Ina maana mume bilionea hajampata.? Nichangamkie fursa.
 
hakuna kitu kizurivkm mwanamke kujua thamani yako,hongera mama mungu akuzidishie
 
Ni vyema mtu kufanya shughuli za maendeleo lakini inabidi pia tuwashauri hawa "celebrities" wetu kwamba maisha yao sio "show" ya kudumu. Si kila kitu wanachofanya basi ni kukikimbiza kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii huku mambo yakiwa ndio mwanzo kabisa. Ndio maana tukianza kujumlisha tuliyoletewa karibuni karibuni kumhusu huyu binti na baadhi ya wenzake tunabaini mikanganyiko. Labda kama mengine wanatuletea kama mizaha kuchangamsha baraza au kutukumbusha uwepo wao pale wanapojikuta si habari ya mjini tena.
 
Back
Top Bottom