Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
HahaaaKuhusudu ni kupenda kupita kiasi,kupenda kwa kutamani,kwahiyo ndugu mpemba anamtamani huyu m chattle(dooh wapemba barna)...husda ni kamati ya roho mbaya,vijicho wasio na huruma! Kama ilivyo kwa Mwenyekiti na Chama Cha Milele
Nami nikifikiri hivyo, ingawaje mifano ysko ni yako mwenyewe.Kuhusudu ni kupenda kupita kiasi,kupenda kwa kutamani,kwahiyo ndugu mpemba anamtamani huyu m chattle(dooh wapemba barna)...husda ni kamati ya roho mbaya,vijicho wasio na huruma! Kama ilivyo kwa Mwenyekiti na Chama Cha Milele
Labda muanzisha uzi muarab wao hawasemi husuda wanasema husda kwa hiyo maneno yote yanaweza kuwa sahihiSamahani sana muanzisha uzi kwanza kabisa hakuna neno Husda bali ni Husuda.
Basi sasa nikirudi kwenye mada tajwa.
1).Husudu;Ni hali ya kupenda kupita kiasi/Sana/kuonea wivu/kuonea kijicho.
Lakini;
2).Husuda;Ni tabia ya mtu kutofurahia mafanikio na maendeleo ya mtu mwingine
Kulingana na kamusi,toleo la tatu,husudu kwanza ina maana mbili.ya kwanza ni kuonea mtu kijicho,na ya pili kupenda mno.na husuda,mleta mada wala si husda.Ni mtazamo Wa ubaya kwa mtu na mali yake.au kutopendezwa na mafanikio ya mtu na kuhisi hastahili.Tumemsikia mzee Mwinyi akisemanana mhusudu JPM.
Mimi nikifikiri kuhusudu ni kupenda kunako ambatana na matamanio.
Bungeni tunasikia maombi ya kutuepusha na husda.
Hapa ni kama kummind mtu kwa nia mbaya.
Waswahili hebu tupeni undani wa haya manenu, husudu na husda.