Sikazi rahisi Rahisi kupunguza maneno ya kiarabu kwenye kiswahili kwa
sababu maneno ni mengi sana kiasi kwamba unaweza ukapewa PHD ya heshima endapo utafanikiwa kufanya
hivyo.
Ngoja niwaongezee maneno mengine 11 ambayo kila mmoja wetu anayatumia kila siku,Haya maneno
tumeyachukua kama yalivyo
1.Tajiri 2.Sukari 3.ghali 4.Rahisi 5.mhandisi 6.robo 7.Nusu 8. kaskazini 9.Kusini 10.Mashariki
11.Maghalibi.
Sahihisho hapo kidogo, neno Kusini kwa kiarabu ni
al-Janūb (الجنوب
😉, na Kaskazini ni
ash-Shamal (الشمال
😉, kama kuna makosa wataalam wanaweza kusahihisha...!
Na neno Magalibi, linaandikwa Hivi:
Magharibi.
Ila ni kweli maneno mengi sana yanatokana na lugha ya kiarabu...! yakiwemo...
Saa, Nia, Kanuni, Katili, Kismati, Kauli, Kiyama, Razi, Salamu, Sababu, Salama, Asubuhi, Taaruki, Taarifa, Jamhuri, Siasa, Dar ES salaam, Alhamisi, Ijumaa, Sifuri, Sita, Saba, Tisa, Arobaini, Hamsini, Sitini, Saba, Sabibi, Themanini, tisini, mia, Alfu, Maji, Bin Adam, binamu, Chemia, Darasa, Chuo, Kanisa, Askofu, Bahari, Amir, adobe, algebra, algorithm, algorism, Alkali, Kahawa, Gitaa, hashish, Jaa, Jasimini, jinn, Safari, Tafsiri, sofa, Spinachi, Sukari, Askari, Sultani Swahili, Mahari, Kitabu, Maktaba, Zahanati, Tarehe, Takriban, Takrima, Umri, Walidi, Wakili, Watani, Yatima, Zalimu, Zani, Zikiri, Ziara, Zulumu, Samaki, Tuna (aina ya samaki), Riwaya, tamthilia, haramia, Jasusi, Sauti, zamani, Dunia, Hatari, Mahali, Msumari, Kata, Habari, Huru, Dhamiri au Dhamira, Kamusi, Baridi, Samahani, rafiki, tafadhali, Furahi, asubuhi, dakika, Mauti, wakati, Alfajiri, alasir, Karne, Tausi, Saidia, Jadi, Kabila, Karatasi, Waziri, Rais, Fedha, Mhasibu, Hesabu, Haki, Dini, Swali, Suhala, Ahsante, shukrani, Thabiti, zaituni, shughuli, Mtihani, Mahakama, Muktasari, thibiti, Ardhi, Adabu, akili, Ashiki, Ajabu, Asiri, Azabu, Awali, Badala, Balaa, Bila, Dawa, Dawati, Dua, Faida, Fakiri, maskini, Tajiri, Fahamu, Faraki, Fikiri, Fitina, Fursa, Ghairi, Hakimu, Halali, Haja, Hakika, Haramu, Hawa, Hawala, Hekima, Himaya, Hukumu, Tabasamu, Hisani, Elimu, Mwalimu, Jahazi, Jeneza, Jawabu, Majununi, Kafiri, katibu, Kalamu, Karimu, Khalisi, Kufuru, Laa, Lazima, Mahiri, Mahaba, Marehemu, Malkia, Msafiri, Mushkeri, Nafsi, Nasibu, Safi, Sharti, Binti, Aghini, Birika, Aibu, Anwani, Afiki, Arusi, Bei, Budi, Deni, Dai, Enzi, Faharasa, Ghasia, Hadi, Ibilisi, Jasho, Kaidi, Madini, Miliki, Naam, radi, Zaidi.
Na mengine mengi ambayo sikuweza kuyakumbuka...
Lakini si Kiswahili tu, ambacho kimetohoa maneno ya kiarabu, hata baadhi ya Lugha kama vile kiingereza, Kispania, Kifaransa, Kireno, na hata Kilatini, pia zimekopa baadhi ya maneno kutoka kwenye Kiarabu, na hii wala si ajabu kwa sababu, lugha kuu karibia zote zimeazimana baadhi ya maneno ambayo kwenye lugha yao hayapo...!