Kama mimi nahama jumla, hela ya matumizi natuma mtu ampelekee mke wangu, simu sipokei wakati mwingine naizima. Nitaona watavumilia hadi lini.
sasa huyo kaka yako anafaidi chakula cha ndoa saa ngapi....?..
inaudhi sana lakini.....
Mi naomba nichangie mambo mawili:
1. Hili si tatizo la ndoa kama ndoa, ni tatizo la uelewa mdogo wa mke wa kaka yako wa namna ya kuihudumia familia yake na mapenzi ya upofu ya kaka yako. Uelewa mdogo na kushindwa kupima uzito wa mambo humpata yeyote aliye kwenye ndoa na asiye kwenye ndoa, hivyo si jema kila baya la ndani ya ndoa lionekana ni tatizo linalosababishwa na ndoa!!! Akili gani ya kumpenda kuhudumia ndugu mpaka unaitesa familia yako mwenyewe?
2. Hapo penye bold ndugu yangu maelezo yako wazi sana kuwa kaka yako haoni taabu na hiyo extended family na mzigo wa kuhudumia hiyo familia. Wewe na ndugu wengine ndo mnaona shida. Mi nakushaurini tu kwa kuwa kaka yako hana taabu ni bora msiiingilie hiyo ndoa, utakuja kuonekana kuwa una chuki na mke wa kaka yako au pengine unataka kubomoa ndoa ya kaka yako. Ndiyo maana mambo mnayomshauri anakwenda kumwambia mkewe mnaanza kuimbiana taarabu ....! Mwache akifunguka akili, atawatafuta yeye mwenyewe!
Kuna wimbo ulikuwa unaimbwa zamani unasema "bibi na bwana wakigombana nyumbani, waache wenyewe mpaka watakapo elewana, lakini usiwangilie eheeee, wakijapatana, utabiki na aibu weee mtoto wa mamaaa"
hawa watu wa hili kabila ni kawaida yao kurundikana kwa ndugu na haijarishi huyo ndugu ana kipato cha kutosha au laah.
mimi na shangazi yangu kaolewa kwenye hilo kabila aisee nyumba yake ikiwa na watu wachache mpaka majirani wanashangaa ni watu 15.........ile nyumba inakuwaga na watu 30........tena mwingine anakuja na mke na watoto wake.......yani sijui wakoje.
wanatesa sana tena wanataka milo yote mitatu waipate..........kuanzia chai asubuh mpaka chakula cha jioni.Sasa Hayo Ni Mateso Jamani!
Umenikumbusha kisa, coincidencially tu kinahusiana na familia ya mke toka Tanga. Baada ya mwezi mmoja tu wa ndoa jamaa aliikutia nyumba yake imejaa kama nyumba ya ndege - wanalala ukumbini, kwenye koridoo, jikoni..... Aliwahi kusema na mke wake lakini huyu alishindwa kuwakataza na kuwafukuza jamaa zake.
Jamaa akaigiza ameanza tabia ya ulevi. Mwanzo alikuwa akirejea nyumbani akiwa "amelewa," anawashambulia mashemeji zake lakini hawa kwa kukosa haya, walikuwa hawajali. La mwisho alilofanya yule jamaa, akirejea anaingia chumbani, akihakikisha wamelala anakwenda anawakojolea. Haikuchukua wiki mbili walihama wote.
sio kuhama, ingekua
mie ningeamka asubuhi nikawaambia kila mtu afunge virago vyake, kuanzia
mke wangu na nduguze, then nawapa nauli nawatakia maisha mema , nitabaki
na wanangu, mke atarudi pale akipata akili......
ila kama huyo kaka anashindwa kufanya hivyo arudi kwake achukue wanae
wapeleke kwa dada yake au wazazi wake au boarding, then humo ndani
asitoe hata shilingi 5 ya matumizi, watakula nini ndo akili itawakaa
sawa