Mi naomba nichangie mambo mawili:
1. Hili si tatizo la ndoa kama ndoa, ni tatizo la uelewa mdogo wa mke wa kaka yako wa namna ya kuihudumia familia yake na mapenzi ya upofu ya kaka yako. Uelewa mdogo na kushindwa kupima uzito wa mambo humpata yeyote aliye kwenye ndoa na asiye kwenye ndoa, hivyo si jema kila baya la ndani ya ndoa lionekana ni tatizo linalosababishwa na ndoa!!! Akili gani ya kumpenda kuhudumia ndugu mpaka unaitesa familia yako mwenyewe?
2. Hapo penye bold ndugu yangu maelezo yako wazi sana kuwa kaka yako haoni taabu na hiyo extended family na mzigo wa kuhudumia hiyo familia. Wewe na ndugu wengine ndo mnaona shida. Mi nakushaurini tu kwa kuwa kaka yako hana taabu ni bora msiiingilie hiyo ndoa, utakuja kuonekana kuwa una chuki na mke wa kaka yako au pengine unataka kubomoa ndoa ya kaka yako. Ndiyo maana mambo mnayomshauri anakwenda kumwambia mkewe mnaanza kuimbiana taarabu ....! Mwache akifunguka akili, atawatafuta yeye mwenyewe!
Kuna wimbo ulikuwa unaimbwa zamani unasema "bibi na bwana wakigombana nyumbani, waache wenyewe mpaka watakapo elewana, lakini usiwangilie eheeee, wakijapatana, utabiki na aibu weee mtoto wa mamaaa"