Wataalam msaada kwenye hili kama lina ukweli ndani yake

Wataalam msaada kwenye hili kama lina ukweli ndani yake

Kwanza tuanzie kwenye chromosomes za jinsia; mke anakuwa na XX, mme ana XY. Yai la mama kabla ya kurutubishwa linakuwa na chromosome X, na mbegu ya baba inakuwa sex chromosome X au Y. Yai la mama likirutubishwa na mbegu ya baba yenye sex chromosome Y basi kiumbe kinachoumbika kitakuwa na maumbile ya kiume kwa sababu hizi: Y chromosome ina sehemu maalum ya kuamrisha utengenezaji wa pumbu (testicle) na baada ya hapo pumbu hizo zitatoa aina ya hormone iitwayo Anti-Mullerian factor ambayo itazuia kuumbika maumbile ya kike.
Uwepo wa chuchu upo kwenye ngozi ambayo huumbwa mapema kabla ya kuumbika kwa pumbu na AMF.
 
Back
Top Bottom