Mtoa mada, huwa ipo hivi.
Kuna kitu kinaitwa Current ambapo unit yake ni Ampere. Na kuna kitu kinaitwa Power ambapo unit yake ni watts.
Sasa, Kwa hapa Tanzania kama load yako( kwa kiswahili kisicho rasmi sana ni kama tuseme uwezo wa vifaa vyako vyote vya kutumia umeme) haitazidi Ampere 60, (13,200 watts)wewe utabakia kuwa ni mteja wa single phase. Lea lugha nyi
Ikiwa load yako itazidi Amperes 60 Basi hapo moja kwa moja utakuwa ni mteja wa three phase. Kwa lugha nyingine ni idadi ya watts katika vifaa vyako vyote kama itazidi watts 13,200 wewe utakuwa ni mteja wa three phase.
Sasa hizo watts unazipataje? Katika kila kifaa cha umeme kina ratings zake. Lea mfano kwenye bulb utakuwa imeandikwa labda 9 W maana yake ni watts 9.
Sasa chukulia labda una pasi, feni, radio, TV, friji, birika la umeme, n.k kila kimoja hapo utajumlisha ili upate total load yako ujue ni kiasi gani.
Kwa summary tu, kama idadi ya watts kwa vifaa vyako vyote haitazidi watts 13,200 wewe utabakia kuwa ni mteja wa single phase.
Idadi ya watts kwa vifaa vyako vyote ikizidi watts 13200 wewe ni mteja wa three phase.
Nawasilisha.