Wataalam "professionals" wa Tanganyika

Wataalam "professionals" wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WATAALAMU "PROFESSIONALS" WA TANGANYIKA WANAFUNZI WA COUNT VICTOR LUSTIG

Uzuri wa Tanganyika ni kuwa unaweza kukodi kila aina ya huduma na kwa kweli fani hii ina wataalamu mabingwa khasa.
Mathalan una jambo lako lakini halinogi sharti uwapate masheikh.

Hawa "wataalamu professionals," watataka kujua ni shughuli gani unata ufanyiwe?

Utawafahamisha mathalan unahitaji masheikh kutoka Bagamoyo waende Dodoma hadi nyumbani kwa mkubwa fulani wakambembeleze achukue fomu za kugombea urais kwa tiketi ya chama fulani.

Hapo utafurahi na nafsi yako.
Wataalamu hawa watakupangia kila kitu.

Watakupatia "masheikh" tena mfano wa watengeneza filamu wa Hollywood wanavyotengeneza "cast."
Hapa ni mfuko wako tu ndiyo unaozungumza.

Utawapata "masheikh," wamevaa kanzu na kofia na watakuwa na viongozi wao nadhifu na pia "masheikh" kanzu mbovu kofia kuchanika.

Wapiga video za online TV wameandaliwa na wenye kazi zao watakuwapo na wahariri wa magazeti watawatoa "masheikh" katika magazeti kama habari kubwa ya siku "Breaking News."

Hapa ndipo tulipo.
Taarifa za kukanusha zitakapokuwa zinashughulikiwa "wataalamu professionals," huwaoni popote.

Kazi yao imekamilika wanatafuta mteja mwingine kutoa huduma yao.
Lakini utasuuzika nafsi yako pale jambo lenyewe linapokuwa la kuigiza lakini igizo lina sura ya kweli kabisa.

Labda utauliza.

Igizo la kweli na lile mathalan la "masheik wavishwa kanzu" nini tofauti yake?
Viko viashiria vingi vitakutanabaisha.

Usibabaishwe na matarumbeta hata kama utamuona Miles Davis ndiyo kiongozi wao.
Angalia wale wanaomfuata nyuma huyu mpiga zumari wa Hamelin.

Utaona wote hao wanaingia kwenye daladala DCM moja bila abiria kusimama ameshika bomba.
Uzuri wa Tanganyika ukiuhangaisha ubongo wako hufi njaa.

We chuna uso wako tu uwe kama uso wa kauzu.

Huyo jamaa hapo chini jina lake ni Count Victor Lustig alipata kuuza mara huo wa Paris mara mbili.

Huyu ndiye baba wa utapeli duniani kote.

1645415218993.png

Count Victor Lustig
 
Hivi wewe mzee umechanganyikiwa au mie ndo sikuelewagi???.....sasa hapa ndo umesema nini....eti utadai ni fasihi andishi.....sawa lkn ya kizamani mnoooo!!.....jaribu kwenda na wkt sawa babu??
 
Hivi wewe mzee umechanganyikiwa au mie ndo sikuelewagi???.....sasa hapa ndo umesema nini....eti utadai ni fasihi andishi.....sawa lkn ya kizamani mnoooo!!.....jaribu kwenda na wkt sawa babu??
Nyaru...
Kutokuelewa ndiyo kunakufanya upoteze adabu yako.

Hujaelewa hurudi na matusi na kejeli.

Hujaelewa unauliza ili uelezwe upate kujua.

Wewe ni umri wa wanangu mimi siwezi kuwa babu yako.

Wajukuu zangu hawajafika umri wako.
 
Back
Top Bottom