Wataalam wa Alibaba: Jinsi ya kuuza bidhaa, Hapa siibiwi kweli?

joe.

Member
Joined
Dec 25, 2013
Posts
36
Reaction score
219
Hbari zenu ndugu zangu. Nilihamasika juzi kati nikapost bidhaa yangu huko Alibaba. Sasa suala ni kuwa nimepata prospective client anataka mzigo huo lakini kwa kiwango kikubwa kuliko hata uwezo wangu wa kusupply. Haina shida nitaoutsource kwa kuwa nahitaji dili.

Tatizo ni kuwa kuna red flags. Kwanza huyo prospective buyer ni from W.Africa, Benin. Pili anataka mzigo wa thamani ya Miln 200. (Ndio millioni mia mbili. Tatu anataka uwe kwa shipping CFR terms. Kiukweli hayo mambo ya CFR, FOB na CIF nayajua sana tu kwa elimu ya darasani ila kwa vitendo ndio naaza kujaribu sijawahi kupractice. Tatu si itabidi niwe na export license nikitumia sea transport kuuza mzigo mwingi hivyo? Wakati mimi ni kijana tu graduate hata kampni sina wala leseni wala hizo export license, ndio kwanza ninjaribu kutoka kwa kuanza na transaction nyepesi?

Tatu, kuhusu malipo. Tanzania hatuna paypal kwa seller. Au mimi ndio sijui? Na pia ninafikiria kumwambia alipe kwanza, tena kupitia western Union or other money transfer ili kuepuka mimi kutuma mzigo bila kulipwa na kupigwa changa. Pia nakwepa kumpa taarifa zangu za bank kwa ajili ya EFT kwa kuwa nahisi inaweza kuwa ni mpango wa kuphish details na kuempty akunt yangu. Je niko sahihi?

Msaada wenu tafadhali wa mawazo. Natanguliza shukrani.
 
Nakushauli mwambie akupe documents za company yake na ukitaka uwe safe tumia ile njia ya L/c
 
banker's acceptance inahusika hapo aiseee... mwambie afanye mpango wa letter of credit ili uwe kwny safe side
 
pole sana mkuu joe hpo lazima uwe makini ila njia za malipo zipo nyingi kuna jamaa aliniambia google pia wana option km paypal ya kupokea hela inaitwa google checkout hii haina longo longo kibongobongo inakubali
 
Sounds intersting..ngoja nijifunze zaidi kuhusu hii kitu pia.
 
Tumia llc mkuu.
Pia ni lazima uwe na co then upate leseni.
Usithubutu kumwambia habari za tt kabla ya mzigo,bcoz kama kweli yupo serious utakua umeua biashara.
Kuhusu mtaji,kuna bank1 ya kiislam ipo hapo dar(nyerere rd)wao wanatoa mtaji kisha mnagawana faida.
Jamaa wapo serious bcoz kuna jamaa yangu alishafanya nao deal.
 
Samahani, by LLC una maanisha nini? Limited Liability Company? Tafadhali kama hutojali, unaweza kushare experience ya jamaa yako?
 
Maelezo yako ni mazuri ila mimi nikuulize tu unauza nini cha 200M toka tanzania ambacho hakina soko la kawaida mpaka uende Alibaba.
 
Back
Top Bottom