Wataalam wa Diagnosis kwenye Magari. Msaada tutani

Wataalam wa Diagnosis kwenye Magari. Msaada tutani

Rweyemam105

Member
Joined
Sep 8, 2012
Posts
69
Reaction score
90
Hallo wana JF.

Najua hapa wamejaa wataalam wa Magari pia.

Mkoko wangu Toyota Allex 2004 Model, ilianza kuwaka taa(Check engine) siku Moja baada ya Kufunga Android radio. Kama kawaida. Nikalazimika kuwaona madokta. Wakaifanyia Diagnosis ika display fault code P0171.

Code ambayo mara nyingi inahusiana na fuel system. Fundi akafuatilia mfumo wote wa Mafuta. Kuanzia buyu la Mafuta, kulisafisha, kusafisha MAF SENSOR, THROTLE, CABURATOR, Tukasafisha Enjector nozzles zote, tukabadili Plugs, bado check engine, inawaka. Especially ukivuta speed hadi 60kmph, ina trigger check engine light. Nimeplan kubadili MAF SENSOR pia.

Je! Ni kipi kingine natakiwa kucheki ili hii fault code P0171 iweze kutoka!?

Please. Kama wewe ni fundi naomba Idea.
 
Upo sahihi iyo ni imbalance mixture ya air-fuel, inatokana na kua na heelwa nyingi mafuta kiduchu kwenye engine.

Tatizo sababu zinaweza kua ni nyingi saaaana: Mfano: vacuum leak (hapa checki leak za pipes hadi intake manifold na gasket), pia inaweza kua MAF kama ulivosema, check Pump, filter, na injectors umesema ushacheki, pia sensor ya oxyg cheki.. ipo too a general
 
Hallo wana JF.

Najua hapa wamejaa wataalam wa Magari pia.

Mkoko wangu Toyota Allex 2004 Model, ilianza kuwaka taa(Check engine) siku Moja baada ya Kufunga Android radio. Kama kawaida. Nikalazimika kuwaona madokta. Wakaifanyia Diagnosis ika display fault code P0171.

Code ambayo mara nyingi inahusiana na fuel system. Fundi akafuatilia mfumo wote wa Mafuta. Kuanzia buyu la Mafuta, kulisafisha, kusafisha MAF SENSOR, THROTLE, CABURATOR, Tukasafisha Enjector nozzles zote, tukabadili Plugs, bado check engine, inawaka. Especially ukivuta speed hadi 60kmph, ina trigger check engine light. Nimeplan kubadili MAF SENSOR pia.

Je! Ni kipi kingine natakiwa kucheki ili hii fault code P0171 iweze kutoka!?

Please. Kama wewe ni fundi naomba Idea.
Mnayaaribu magari kwa kuweka hizo Android Radio
 
Hallo, wana JF,


Nimerudi na Mrejesho, ili iwe kama "Precedent" kama mtu atakayekutana na tatizo kama langu nlilo address hapo juu, lilosababisha check engine kuwaka na kupelekea ECU kusoma Fault code P0171 kwa kitaalamu hiyo Fault code inafahamika kama. "System is too lean." Yaani kiwango cha upepo kwenye engine Combustion ni kingi kuliko mafuta. Yaani hamna uwiano wa Upepo na Mafuta yanayo hitajika kwenye engine Combustion.


Opposite yake ni Fault code P0172 ambayo kitaalamu hujulikana kama "System is too rich" yaani hii fault code hupelekea kiwango cha Mafuta kuwa mengi kuliko upepo kwenye engine.. Sasa basi katika pita pita zangu kutafuta msaada wa mafundi.


Nikakutana na Mafundo waliotaka kumaliza shida na madeni yao kwenye tatizo langu.


Fundi mmoja nilimuulezea tatizo, akanambia, hiyo ni kazi rahisi. Nimtafutie laki6 ili aweze kutatua hiyo shida.


Fundi wa Pili akataka laki3.5 na Gari awe Nayo kwa siku kadhaa.
Fundi wa tatu akanambia gharama yake ni laki 4 spare ataniandikia.


Nikatahamaki, nikajiuliza je ni engine tunashusha!?


Nikajiendea kwenye kijiwe ambacho huwa nafanya regular service mara kwa Mara. Nikamuelezea namna gari inavyo behave. Akaipima na OBDII. Ikaleta Fault Code ile ile P0171. SYSTEM IS TOO LEAN. tukaingia Google. Na kucheki possible causes.


Tukapanga kuanza kubadilisha/kufanyia kazi kipengele kimoja baada ya kingine. Infact, kulikuwa na vipengele kama 06, possible causes ambavyo tulitakiwa kuvi address.


Tukaanza na


1. Kubadili Plugs, zilizokuwepo sikuwekewa saizi yake. Tatizo halikuisha.





2. Tukasafisha MAF SENSOR(Airflow Sensor) tatizo halikuisha.





3. Tukasafisha Nozzles/injections na Throtle, O2 sensor. camshaft sensor, Tatizo halikuisha.





4. Tukakagua intake manifold kama iko na leakage. Haikuwa na Leakage. Bado check engine ikawa inawaka kuashiria kuwa tatizo bado liko pale pale.



5.Tulifuatilia System yote ya Mafuta, ikiwa ni kuanzia kwenye fuel tank, kuona labda kama kuna hitilafu. Tukatoa buyu la mafuta na Pump yake, likasafishwa, na kurejeshwa vzuri. Bado check engine ikaendelea kuwaka. Ningekuwa na gari ya pili, hii ningeiuza kwa bei ya hasara. 😂


6. Binafsi mm sio Fundi, ila napenda kujifunza mambo ya Magari esp kwenye mechanics namna gari inavyo operate. Na basics ndogo ndogo, just incase nikipata shida njiani nijue pa kuanzia. Pia kwenye upande wa IT sijasoma ila siwezi kulala bila kuperuzi na kujifunza jambo jipya la kitechnolojia kwenye mtandao. Hadi chuo mwalimu wangu wa Computor Knowledge alihisi pengine nimesoma computer kwa level za juu. Nikawa namkatalia, kuwa ni maarifa napenda kuchota kwneye mtandao. To cut a story. Jioni moja nikiwa naperuzi. Nikakesha na somo la Fault code P0171 system is too lean. Kesho yake nikamwambia Fundi. Nimegundua tatizo linaweza kuwa wapi. Akaniambia niende. Nlipofika. Nikamwambia, aipime gari fuel ⛽ pressure. Alivyo pima, pale pale tukabaini, fuel pressure ilikuwa ni ndogo tofauti na kiasi kilichokuwa kinahitajika kuwa pumped kwenye engine combustion. Tukafungua Buyu la mafuata kwa Mara nyingine, tukaisafisha Fuel filter, tukaitoa Pump. Tukaweka Fuel pump mpya baada ya kujaribu kama 3 ambazo ni used, lakini tatizo la pressure likawa bado pale pale. Tukaamua kufunga mpya. Tulipokamilisha. Tukawa tumemaliza tatizo kwa gharama hata laki na nusu haikufika. 😂



Hivyo basi, tatizo lilisababishwa na fuel pump, ilikuwa imechoka na kushindwa ku ejaculate ratio nzuri kiwango cha mafuta yanayohitajika kwenye engine Combustion 🤣. Gari ilikuwa ikifika speed 60kmph, ina trigger check engine. Au ukipanda kilima kidogo tu kwa speed hata ya 30kmph, check engine ilikuwa lazima iwake.


Emagine hapo Fundi ashakwambia anataka laki 6 ili aweze kutatua hiyo Fault code P0171. Ni kweli mafundi wamesoma kwa shida. Ila tusiwaumize wateja kwa vile tu uko na shida na unataka ku solve matatizo yako kwa kazi moja tu.
 

Attachments

  • 20250210_182114.jpg
    20250210_182114.jpg
    238.3 KB · Views: 4
  • 20250210_182110.jpg
    20250210_182110.jpg
    303.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom