Mimi nadhani kabla hujanunua hisa ningekushauri kwanza ujielimishe kuhusu dhana nzima ya hisa na vitu gani vinavyofanya hisa zipande au kushuka. Nasema hivi kwa sababu hata hizo hisa utakazoambiwa uzinunue leo kwa kuwa zinafanya vizuri, hakuna guarantee kwamba kesho na kesho kutwa zitaendelea kufanya vizuri vile vile. Hili likitokea si ajabu utarudi na kuwalaumu waliokushauri uzinunue kwamba wamekudanganya. Kumbe hata wao wasingejua.
Kabla hujawekeza mahali - hasa kwenye mambo kama haya ya hisa, bonds..., hakikisha kwamba una maarifa na habari sahihi kwanza...