Biashara ya kufuga kuku imekua ndoto yangu ya mda mrefu. Katika kuitimiza ndoto hii niliamua kuanza kufuga kuku wa mayai yaani layers. nilianza kwa kujenga banda zuri la kisasa. Nilianza na vifaranga miatatu. Nilifanikiwa kuwakuza vizuri sana kwa kuzingatia chanjo ambazo ni ya gombola na ile ya newcastle kuku walistawi vizuri na ilipofika mda wa miezi minne na wiki mbili wakaanza kutaga. Walitaga vizuri mpaka wakafikisha wastani wa trei 8 kwa siku..biashara ikanivutia kwa kweli nikaamua kupanua mradi kwa ujenzi wa banda lingine.. mara baada ya miezi miwili ya utagaji kupita kuku wakaanza kupunguza utagaji nikaamua kuchukua sampo ya kuku kwenda kupima . daktari akasema wamepata typhod. akanipa garadex kiukweli haikusaidia. kuku wakawa wanapungua uzito kwa kasi na wakawa wanakufa.. Nikazunguka kwa madaktari wengi lakini haijasaidia mpaka mimi mwenyewe nilipoamua kupitia kwenye mitandao ndipo nikapata ushauri wa kutumia tetracycline.. zikasaidia sanaa. ingawaji kuku walikufa na kubakia 100. Nakaribisha michango juu ya njia za kukabiliana na typhod na fawl cholera kutoka kwa wadau.. na je kunachanjo yoyote juu ya haya magonjwa??