Wataalam Wa Kufuga Kuku nichangieni Mawazo..

NNKOSON

Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
50
Reaction score
24
Biashara ya kufuga kuku imekua ndoto yangu ya mda mrefu. Katika kuitimiza ndoto hii niliamua kuanza kufuga kuku wa mayai yaani layers. nilianza kwa kujenga banda zuri la kisasa. Nilianza na vifaranga miatatu. Nilifanikiwa kuwakuza vizuri sana kwa kuzingatia chanjo ambazo ni ya gombola na ile ya newcastle kuku walistawi vizuri na ilipofika mda wa miezi minne na wiki mbili wakaanza kutaga. Walitaga vizuri mpaka wakafikisha wastani wa trei 8 kwa siku..biashara ikanivutia kwa kweli nikaamua kupanua mradi kwa ujenzi wa banda lingine.. mara baada ya miezi miwili ya utagaji kupita kuku wakaanza kupunguza utagaji nikaamua kuchukua sampo ya kuku kwenda kupima . daktari akasema wamepata typhod. akanipa garadex kiukweli haikusaidia. kuku wakawa wanapungua uzito kwa kasi na wakawa wanakufa.. Nikazunguka kwa madaktari wengi lakini haijasaidia mpaka mimi mwenyewe nilipoamua kupitia kwenye mitandao ndipo nikapata ushauri wa kutumia tetracycline.. zikasaidia sanaa. ingawaji kuku walikufa na kubakia 100. Nakaribisha michango juu ya njia za kukabiliana na typhod na fawl cholera kutoka kwa wadau.. na je kunachanjo yoyote juu ya haya magonjwa??
 
nakutakia kila la heri mkuu.
 
Cha Muhimu Banda liwe safi na kavu
Kuku hawatabukizwa magonjwa hovyo
 
Kinga ni bora kuliko tiba, hakikisha banda na kuku wapo katika mazingira safi. Hiyo Tetracycline nadhani ndio tiba bora zaidi.
 
Pole sana kuku wanaotaga zaidi ya mia kufa ni issue. Hapa kuna mawili umelegeza kanuni za usafi, umebadili mtu au amechoka hasa kama umemwongezea kazi bila kuongeza mshahara. Wanakosa Chakula bora na vitamin kuwapa kinga. Kama ulilea vifaranga hadi kutaga nadhani uzoefu umepata kuongezea tu
*usafi wa vyombo na banda na maji, tumia water guard ikibidi. Vyombo osha na disinfectant mara moja kwa mwezi. Tumia footbath au usiingize wageni au viatu bandani
*kinga wape vitamin na antibiotic mara moja moja nadhani famasi wanayo ratiba au muulize Zanstan
*wakiumwa tu au kupungua kutaga kagua na watenge wagonjwa haraka. Angalia dalili zote maana famasi nao binadamu wanakisia
*jaribu kuwa karibu na biashara kujua masharti yanafuatwa, pia toa motivation kwa staff au badili ikibidi. Usikate tamaa kila la heri
 

Thanx kwa ushauri mzuri inaonekana ni mzoefu kwenye hii biashara.. ila hujagusia kuhusu chanjo ya fawl cholera na typhod.. zipo kweli na zinafanya kazi?
 
pole mkuu zingatia usafi wa vyombo na mazingira.ila tambua kuwa antibiotic ni sehemu ya chakula cha kuku hvyo jiwekee ratiba hata mara moja kwa wiki.
 
Thanx kwa ushauri mzuri inaonekana ni mzoefu kwenye hii biashara.. ila hujagusia kuhusu chanjo ya fawl cholera na typhod.. zipo kweli na zinafanya kazi?
Fowl typhoid haina chanjo ila inatibika na kuzuilika jitaidi tu maji kama sio ya bomba weka water guard, mara kwa mara wape vitamin au premix huwa zina dose za antibiotic Fulani lakini pia kuna ratiba hawa kuku wanapewa dose ya antibiotic bila kusahau chanjo ya Newcastle kila miezi 3, hii ni muhimu na ni ugonjwa unaoua sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…