Wataalam wa Sayansi wanapostaafu

Wataalam wa Sayansi wanapostaafu

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Mwaka juzi nilimtafuta Prof Mmoja aliyekuwa Chuo, nilienda kuomba ushauri fulani wa Kilimo, nikaambiwa amestaafu na kuchukuliwa na Wizara ya Kilimo Nchini Zambia kama mshauri mkuu.

Nikawa nawazia kuwa wataalamu kama hao ni vizuri kuwafuatilia na kunufaika nao kwa kadri inavyofaa.

Mfano: Wataalamu wanaojihusisha na utafiti wa Mbegu, magonjwa na mimea, Waganga wa mifugo nk.

Nakumbuka, kuna Doctor mmoja wa Mifugo (nafikiri ana Diploma yule) aliniambia ametibu mifugo kwa takribani miaka 25 na ndio amestaafu anasema; baadhi ya dalili za magonjwa ya mifugo zimebadilika sana ukilinganisha na zinazofundishwa vyuoni.

Nafikiri ipo haja ya kutengeneza mazingira ya kupata feed back ya wataalam walichojifunza wakati wa kutekeleza majukumu yao hadi kustaafu na kupewa nafasi ya kupendekeza maboresho.

NK NK NK
 
Wataalamu wengi wa Tanzania sijui kwanini hawana hata kitabu walicho andika. Wapowapo tu
 
Wataalamu wengi wa Tanzania sijui kwanini hawana hata kitabu walicho andika. Wapowapo tu
Mkuu, sio Tanzania tu bali takriban ni duniani kote.

1. Wataalam wengi wanapo staafu hujikuta wanaanza aina ya maisha mapya tofauti na kazi za Ofisini e.g. hakuna routine work kama za Ofisini, Hakuna mtu(Boss) anayekufuatilia utendaji wako i.e. husukumwi na yeyote kufanya jambo/kazi n.k. na hatimaye kutolea Taarifa ya ulichokifanya.

2. Wengi hujikuta mwisho wa mwezi wanapata kitu kidogo sana (pension tu) ukilinganisha na alichokuwa akipata alipokuwa Ofisini/mwajiriwa (Mshahara , Night Outs, Allowances, n.k......Kutokana na hilo wengi wanakuwa ni wahangaikaji lakini ramani hazisomi kwa hiyo hawana utulivu wa kuweza kuandika vitabu. Hata hivyo wataandika kwa ajili ya nani?

3. Wengi huwa frustrated kutokana na ile hali kwamba hawana Umaarufu tena katika Jamii na ndo mana hata ww unasema wapowapo tu.

4. Wengi wanakuwa Localised/sedentary i.e. Huwa hawasafiri-safiri sana na muda mwingi wanaonekana kana kwamba wameridhika - sio wachakarikaji kwani kila anachofikiria kinakuwa kama ni too late.
 
Mkuu, sio Tanzania tu bali takriban ni duniani kote.
1. Wataalam wengi wanapo staafu hujikuta wanaanza aina ya maisha mapya tofauti na kazi za Ofisini e.g. hakuna routine work kama za Ofisini, Hakuna mtu...
Nafikiri sio kwa dunia nzima kwani wenzetu (Ulaya na marekani) watu wa Saiyance kwa waliosoma vizuri hadi kupata PhD huwa hawastaafu, huachwa hadi wapoteze uwezo wao wa kufanya kazi husika.

Wakisha kuwa watu wazima hutumiwa zaidi kwenye utafiti na ushauri katika idara husika.

Nimeona umetoa hoja tofauti tofauti ila hujatoa utatuzi wake!
 
Nafikiri ipo haja ya kutengeneza mazingira ya kupata feed back ya wataalam walichojifunza wakati wa kutekeleza majukumu yao hadi kustaafu na kupewa nafasi ya kupendekeza maboresho. La
Naunga mkono hoja hii
 
nafikiri sio kwa dunia nzima kwani wenzetu ( Ulaya na marekani) watu wa Saiyance kwa waliosoma vizuri hadi kupata phD huwa hawastaafu, huachwa hadi wapoteze uwezo wao wa kufanya kazi husika...
1. Wataalam waliostaafu (isiwe ni kwa wanasayansi tu bali kwa fani zote) wangebaki kama "Consultants" na kila anapohitajika katika shughuli inayohusu fani yake awe analipwa.

2. Pensheni ingefaa iangaliwe kama mojawapo ya kipato kwa mstaafu. Kwa mantiki hiyo kuwepo na ongezeko la kiwango (Increments) kama ilivyo kwa watumishi serikalini i.e.mshahara huongezeka-hupanda, ingekuwa hivyo hivyo na kwa wastaafu ili mstaafu aweze walao kukabiliana na hali ngumu ya maisha badala ya kiwango anachopokea kubaki ni kile kile mwaka hadi mwaka.

3. Wastaafu waruhusiwe - Serikali iweze kuwaajiri kwa masharti ya muda au Part time kwa sababu ki-ukweli wapo wastaafu waliostaafu kwa sababu ya umri tu kusoma ni 60yrs lakini bado wana uwezo mkubwa, nguvu na ari kubwa hata kushinda hawa new employees.

4. Serikali iwatake Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuanzisha mfumo wa kuwajengea uwezo (capacity building) wastaafu waliochangia katika mifuko husika e.g. PSSSF, NSSF n.k badala ya kuwatelekeza na kuachia Taasisi nyingine za kifedha e.g. Mabenki, Mashirika na Vikundi vya kuweka na kukopa ndo vishughulike nao.

Wanasahau Fedha waliyo nayo imetokana na michango ya hao watumishi - Wangelirudisha walao fadhila badala ya kuzingatia Biashara tu.
 
Mkuu, sio Tanzania tu bali takriban ni duniani kote.

1. Wataalam wengi wanapo staafu hujikuta wanaanza aina ya maisha mapya tofauti na kazi za Ofisini e.g. hakuna routine work kama za Ofisini, Hakuna mtu(Boss) anayekufuatilia utendaji wako i.e. husukumwi na yeyote kufanya jambo/kazi n.k. na hatimaye kutolea Taarifa ya ulichokifanya.

2. Wengi hujikuta mwisho wa mwezi wanapata kitu kidogo sana (pension tu) ukilinganisha na alichokuwa akipata alipokuwa Ofisini/mwajiriwa (Mshahara , Night Outs, Allowances, n.k......Kutokana na hilo wengi wanakuwa ni wahangaikaji lakini ramani hazisomi kwa hiyo hawana utulivu wa kuweza kuandika vitabu. Hata hivyo wataandika kwa ajili ya nani?

3. Wengi huwa frustrated kutokana na ile hali kwamba hawana Umaarufu tena katika Jamii na ndo mana hata ww unasema wapowapo tu.

4. Wengi wanakuwa Localised/sedentary i.e. Huwa hawasafiri-safiri sana na muda mwingi wanaonekana kana kwamba wameridhika - sio wachakarikaji kwani kila anachofikiria kinakuwa kama ni too late.
Hiyo namba nne inaathiri wengi. Wengi tu. Mtu ana miaka 60 kastaafu udaktari anafikiria kwenda kuanzisha dispensary au pharmacy wakati anaona zingine zimeshamiri. Anaona kachelewa.
 
Back
Top Bottom