Paragumu
JF-Expert Member
- Dec 8, 2014
- 326
- 142
Habari za Jumapili waungwana,jamani naomba wataalam wa sheria mnisadie kwa hili.
Nafaham kuwa kwenye nyumba za kulala wageni kuna vitabu vya kusajili kila mgeni anayelala kwenye nyumba hiyo na ni ukweli usiopingika kuwa ni jambo jema kwa kila upande.
Lakini msaada ninaohitaji ni kufahamishwa ni kosa kupitia sheria ipi kuwa usipoandika jina waweza kushitakiwa mahakamani na adhabu yake ikoje. Nimeuliza hili kwa kuwa nimekuwa nikishuhudia wateja wenzangu wakipata shida mara msako unapopita na huwa sijui kesi hizo zinaishaje.
Sambamba na hili nimeshuhudia mteja ameandika jina kwenye kitabu lakini polisi wakambeba kwakuwa wametaka awaoneshe kitambulisho bahati mbaya hakuwa nacho.
Kama mada hii ilishawahi jadiliwa humu naomba nipewe link ili nisisumbue waungwana nikaisome moja kwa moja.
Naomba kuwasilisha.