Wataalamu naomba kufahamu Puto tumboni na Vyuma kwenye moyo wa binadamu

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Wakuu habari za muda huu hapa ubaoni.
Leo kwa hisani yenu naomba wataalamu wa masuala ya afya au yeyote mwenye kufahamu masuala haya, anijuze kuhusu vyuma kwenye moyo wa binadamu na puto tumboni.

Leo 10 Novemba 2017, mahakama ya Kisutu imeambiwa kuwa Puto lililopo tumboni kwa Seth limeisha muda wake na linaweza kupasuka muda wowote, hivyo aruhusiwe kuonana na daktari wake wa Afrika Kusini kwa kuwa Muhimbili haina uwezo wa kumtibu.

Mwezi uliopita taarifa ya daktari iliiambia mahakama kuwa Mfanyabiashara Yusuf Manji, moyo wake una vyuma vinne na yuko kwenye hatari kiafya, anatembelea kamba nyembamba.

Tumshukuru Mungu kwa kutupa uzima, maana hakuna neema kubwa kama uzima ugonjwa wa moyo upo ila kwanini sasa ishabihiane na vyuma au kuumwa tumbo halafu ishabihiane na puto.

Puto tumboni na vyuma moyoni ni nini hasa. Na husababisha na nini? Wataalamu wabobezi kwa hisani yenu tuwekee wazi tafadhali.

Nawasilisha
 
Puto tumboni ni haya ya kupuliza hasa huwa wanayapenda watoto..huwa likipulizwa likijaa upepo linasababisha vitambi...ndo maana Seth anakitambii...
Msemo wa vyuma vimekaza...hivyo ndo vyuma vilivyopo moyoni..ukimsikia mtu anasema vyuma vimekaza mwambie akuonyeshe..
 
Mkuu wewe umetania tu tucheke hapa. Lakini kuna watu wanaoumwa.
 

Ukishakula sana hela za umma sababu ni nyingi lazima uongoze puto ili zipate sehemu ya kukaa.
 
Pumba mbichi, maharage mtindi ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…