#COVID19 Wataalamu nisaidieni: Hivi ni sahihi kuanzisha kodi mpya katikati ya janga la Corona?

#COVID19 Wataalamu nisaidieni: Hivi ni sahihi kuanzisha kodi mpya katikati ya janga la Corona?

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
2,427
Reaction score
4,944
Kwanza naomba ku-declare interest. hii serikali siipendi.

Baada ya hapo niende kwenye mada moja kwa moja.

Baada ya kifo cha kiongozi wetu aliekuwa anazipinga waziwazi conspiracy theories karibu zote zinazohusu corona. Mrithi wake kaja na wazo tofauti. yeye anazikubali pamoja na mambo yake yote.

Ni vile tu anaona aibu ila kimoyomoyo anatamani tufungiwe ndani lockdown.

Na hakuna ubishi kuwa janga la corona ni baya. ushahidi upo wazi nchi za magharibi zimeumia pakubwa. hata sisi tumeumia ila kwakuwa serikali yetu inaendeshwa kwa 99% uongo 1% kweli basi kila mtu hana data kamili za damage.

Swali langu ni je, serikali ipo sahihi kiasi gani kuanzisha aina mpya ya kodi katikati ya janga la corona ambalo linatafuna uchumi wa dunia nzima?
 
Ni swali nzuri ila Mama anasema anashughulikia uchumi kwanza mambo mengine baadaye (akishastaafu).
 
Nchi za wenzetu janga la Covid lilivo wavamia walipunguza "KODI na RIBA ZA MIKOPO (Tax and Loan Interest Waver", ili kupunguza biashara za raia wao sambamba na uchumu wa nchi zao usiathirike sana. Ila athari ilikuwepo japo ilipunguzwa makali.

Na kuna baadhi ya nchi walikwenda mbele zaidi na kuamua kuwalipa "POSHO YA MWEZI" kila raia aliefikisha umri wa miaka 18.

Tanzania viongozi na wabunge walivyo majuha ndio kwanza wamepandisha;

1) Kodi Kwa Wavuvi (2%).

2) Kodi Kwa Wakulima.

3) Kodi Na Tozo Kwa Miamala Ya Simu (Haina Haja Hata Ya Kuichambua)

4) Kodi Kwenye Zana Za Kilimo (Kodi Kwenye Mbolea).

[emoji830] Mbolea Ya Kupandia DAP imepanda kutoka 52,000/=Tsh mpaka 92,000/=Tshs.

[emoji830] Mbolea Ya Kukuzia UREA imepanda kutoka 48,000/=Tshs mpaka 80,000/=Tshs.

[emoji830] Mbolea Ya Kukuzia CAN imepanda kutoka 40,000/=Tshs mpaka 60,000/=Tshs.

5) Kodi Ya Mafuta (Petrol & Diesel).

[emoji830] Mafuta Mpaka Kufikia Bandari Ya Tanzania yanasimama "Sh 1,160/=Tshs Kwa Lita 1". Halafu yanakutana na "Kodi za aina 23" tofauti tofauti mpaka kufikia "Sh 2,405/=Tshs kwa lita 1".

[emoji830] Wharfage Sh 20.60/=Tshs.

[emoji830] Railway Dev Levy Sh 17.40/=Tshs.

[emoji830] Custom Processing Fee Sh 4.80/Tshs.

[emoji830] Weights & Measure (WMA) Fee Sh 1/=Tshs.

[emoji830] TBS Charge Fee Sh 1.20/=Tshs.

[emoji830] TASAC Fee Sh 3.50/Tshs.

[emoji830] EWURA Fee Sh 6.10/=Tshs.

[emoji830] Fuel Marketing Sh 14.1/Tshs.

[emoji830] Demurrage Cost Sh 5.50/=Tshs.

[emoji830] Surveyors Cost Sh 0.18/=Tshs.

[emoji830] Financing Cost Sh 11.60/=Tshs.

[emoji830] Evaporation Cost Sh 5.80/=Tshs.

[emoji830] Fuel Levy Sh 413/=Tshs.

[emoji830] Excise Duty Sh 379/=Tshs.

[emoji830] Petroleum Fee Sh 100/=Tshs.

[emoji830] Oil Marketing Companies Margins (Profit) Sh 123/=Tshs.

[emoji830] Charges Payable Sh 5.44/=Tshs.

[emoji830] Transport Charges Local Sh 10/=Tshs.

[emoji830] Service Levy Sh 6.10/= Tshs.

Kutoka kwenye Sh 1,160/=Tshs kwa lita moja inapanda mpaka kuwa Sh 2,405/=Tshs kwa lita moja (Hii ni kwa Dar Es Salaam tu, mikoani inakua zaidi).

"CCM Hoyee, CCM Hoyeeee. Hatutaki kusikia mtu analilia Katiba Mpya Mpaka Akili Zikae Sawa Kwanza!!! Msiokua na magari ondoeni ndoto za kuja kumiliki gari kabisa!!!"
 
Haipo nchi hata moja iliyo waongezea kodi achilia mbali kutowapunguzia mzigo wa kodi wananchi wake kwenye janga hili.

Nchi zingine zikiwamo hapa EA zimegawa pesa, chakula na hata kufuta kodi kabisa kwenye kipindi cha janga hili.

Hata mkoloni asingethubutu kuongeza kodi ila mkoloni mweusi.
 
Mafuta bei juu,
Mawasiliano bei juu
Huduma za pesa bei juu.
Mbolea bei juu
Ushuru wa magari juu
Na vyoote hivi vinagusa maisha ya watu wote.
Wao KILA kitu bure na awakatwi kodi hivyo hawawezi kuwa na uchungu.
 
Ni hatari kwa wananchi kutawaliwa na watu waliojigeuza wakiloni. Katika hali ngumu ya uchumi kama hii kuongeza kodi ni dharau kwa wanchi.

Hata matumizi yake utasikia ni ujenzi wa miundo mbinu

Hivi kwenye hali hii ni lazima kujenga mabarabara
 
Yes. But only in sisi tu tanzania kwa watu wajinga na wenye uchumi wa kati
 
Mna anzisha miradi ya matrillion na hela hamjui pa kuzipata, kwanza wafanyakazi wa uma tumelipa kodi nyingi kwa unyenyekevu muda mrefu kwa hiyo vumilieni tu
 
Back
Top Bottom