Mkuu kwa utaratibu wa kawaida wa kibenki hauwezi kupewa mkopo kwa kutumia majengo ambayo hayana hati kwa kuwa sheria ya mikopo yenye dhamana (tafsiri isiyo rasmi ya mortgage financing act 2008) hairuhusu. Lakini unaweza kufuata utaratibu wa business proposal ukapeleka kwa taasisi zinazotoa mkopo na mkaingia makubaliano ya kisheria. Au njia rahisi tafuta makampuni yanayojihusisha na kudevelop properties wape proposal wanaweza kukusaidia. Na lastly weka dhamani mali zako nyingine ili uweze kukopesheka, waweza kutumia nyumna yako nyingine au mtafute mtu akudhamini kwa mali zake.