Wataalamu wa fashion: Watu wanaweza kulingana kimo hadi rangi lakini ...

Wataalamu wa fashion: Watu wanaweza kulingana kimo hadi rangi lakini ...

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari za jumapili wana JF.

Katika masuala ya mavazi kuna mambo Mengi sana. Unakuta watu wamelingana kimo kila kitu hadi rangi na hata hadhi ktk jamii. Lakini wanapovaa kuna mmoja anasifiwa sana kuliko mwenzie, cha ajabu hata akivaa kiatu, nguo mtumba na chochote kile yeye huwa anafunika kwa uzuri au utanashati.

Hii ni huwa inatokea kwa jinsia zote yaani wanaume na wanawake kiasi kwamba mtu huyu watu huanza kushindananaye kwa kumuiga.

Hali hii husababishwa na nini ilihali watu wengine ukiwatazama wamelingana kila kitu?
 
Sijuagi ni kitu gani kuna kipindi had mtu unaweza hisi wanakukejeli, cz ukiangalia kutoka juu had chini hujavaa kitu kizurii kiivyo lakini utasikia umependeza,
Cha ajabu siku nikaamua niende ktk.mitaa ya wenye hela zao nikasuka mabutu yangu tu ya hovyo hovyo, na make up sipakagi, mtu akapita akasema umependeza sasa najiangalia sioni kitu aisee nikacheka kwa nguvu nikasema hawa wananisanifu sasa

Nimegundua kitu kuna watu hata avae hovyo nguo itamkaa tu hata kama hana shape zetu pendwa wapendazo wakaka, hata wakiwa moja wakivaa mtumba dukani.ndala au viatu bado wana ule muonekano fulani hivi mzuri

Na sio kuwa wanakuwa wazuriiii hapana, wapo attractive zaidi

Kwa wakaka mtu anakuwa na umbo la kiume, hivyo kila nguo inamkaa, hata kama ana sura ambayo normal lakin akivaa nguo anamkaa kiume

Sio mtaalam kwenye mavazi wala urembo naongelea tu ya mtaani niyaonayo
Kingine . Watu wa aina hii anaweza akawa na nguo chache sana, lakin kila akivaa utaona bado ipo vzr zaidi ya jana na atakuwa na mvuto tofauti na wa jana. Na hawana shida ya kuchagua avae nguo ipi wao kila nguo inawakaa tu

Kwanini? Hata mimi.sijui
 
Back
Top Bottom