Sijuagi ni kitu gani kuna kipindi had mtu unaweza hisi wanakukejeli, cz ukiangalia kutoka juu had chini hujavaa kitu kizurii kiivyo lakini utasikia umependeza,
Cha ajabu siku nikaamua niende ktk.mitaa ya wenye hela zao nikasuka mabutu yangu tu ya hovyo hovyo, na make up sipakagi, mtu akapita akasema umependeza sasa najiangalia sioni kitu aisee nikacheka kwa nguvu nikasema hawa wananisanifu sasa
Nimegundua kitu kuna watu hata avae hovyo nguo itamkaa tu hata kama hana shape zetu pendwa wapendazo wakaka, hata wakiwa moja wakivaa mtumba dukani.ndala au viatu bado wana ule muonekano fulani hivi mzuri
Na sio kuwa wanakuwa wazuriiii hapana, wapo attractive zaidi
Kwa wakaka mtu anakuwa na umbo la kiume, hivyo kila nguo inamkaa, hata kama ana sura ambayo normal lakin akivaa nguo anamkaa kiume
Sio mtaalam kwenye mavazi wala urembo naongelea tu ya mtaani niyaonayo
Kingine . Watu wa aina hii anaweza akawa na nguo chache sana, lakin kila akivaa utaona bado ipo vzr zaidi ya jana na atakuwa na mvuto tofauti na wa jana. Na hawana shida ya kuchagua avae nguo ipi wao kila nguo inawakaa tu
Kwanini? Hata mimi.sijui