Wataalamu wa Green House

MrIsidori

Senior Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
191
Reaction score
83
Naomba kujua ukishajengewa green house mfano ya nyanya inakaa mda gani? [nina maana how long period it lasts? ] Natanguliza Shukrani kwenu!
 
Unaanza kuvuna miaezi mitatu baada ya kuzipanda. Utaendelea kuvuna kwa miezi 8 hadi 11. Ingia Google kuna material mengi kuhusu greenhouse, au ingia Youtube uangalie, kama ngeli inapanda utaelewa huko. Mimi mwenyewe nimalizia kuweka miundombinu sawa ili nianze kulima
 
Naomba kujua ukishajengewa green house mfano ya nyanya inakaa mda gani? [nina maana how long period it lasts? ] Natanguliza Shukrani kwenu!

Ngoja mkuu tukuitie Sanctus Mtsimbe aje akudadavulie hapa kuna kipindi aliwahi kuleta mada hapa jamvini ya kuhusu kilimo cha kutumia Green House. Ukijaribu kuitafuta hiyo mada hapa jamvini utaipata!
 
Swali langu la msingi ni kwamba nikishajengewa hiyo green house, itadumu kwa mda gani ili nijengewe nyingine mpya?
 
Inategemea umejenga ya aina gani, ukitumia chuma inakaa hata 15 years but kama ni miti depending na. Type ya mti hata 4years
 
Vp sheets unaweza tumia turubai? na zile za net zikoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…