Wataalamu wa historia, nchi gani ulimwenguni imewahi kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu?

Wataalamu wa historia, nchi gani ulimwenguni imewahi kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu?

okonkwo jr

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2015
Posts
2,419
Reaction score
1,738
Binafsi siamini kilichotokea Zanzibar, naona kama ndoto vile. Je, kuna wataalamu wa historia ambao wanaweza nambia nchi yeyote duniani ambayo imewahi kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu tofauti na nchi ya Zanzibar?
 
Hakuna huwa yanafutwa ya ubunge tuu wamefanya ivo kwa sababu upinzani wameshinda
 
Zanzibar siyo nchi ni mkoa ambao RC wake anapatikana kwenye sanduku la kura na kupachikwa jina la rais.Ni wapi uliona chama cha siasa kisajiliwe nchi A halafu kikashiriki uchaguzi nchi A na B kwa usajili wa nchi A? Au Zanzibar nao hu-re-register hivi vyama?
 
Historia inatujulisha kuwa uchaguzi wa February 1986 wa nchini Phillipines ulifutwa baada ya shinikizo toka nchi za nje pamoja na wananchi na viongozi wa jeshi la nchi yao baada ya Rais Marcos kuonekana dhahiri ameshinda kiti cha Rais kwa kuchakachua takwimu. Baada ya kufutwa matokeo hayo mshindi wa pili Corazon Aquino alitangazwa ndiye mshindi wa kiti cha Rais.

Vile vile historia inatueleza kuwa baada ya kubaini kuwa uchaguzi hautakuwa wa huru na wa haki walisusia kwenda kupiga kura. Mwaka 1983 asilimia 97.3 (97.3 %) ya wananchi wa Jamaica walisusia kwenda kupiga kura na tume iliona aibu kutangaza matokeo yatokanayo na 2.7 % ya wapiga kura. Mwaka 1997 asilimia 90.5 (90.5 %) ya wananchi wa Slovak walisusia kwenda kupiga kura na tume iliona aibu kutangaza matokeo yatokanayo na 9.5 % ya wapiga kura.

Refer: https://en.wikipedia.org/wiki/Philippine_presidential_election,_1986

Refer:https://en.wikipedia.org/wiki/Election_boycott
 
Thanks
 
hili la zanzibar, litatutafuna daima... Kweli kama wananchi tusipohoji huu ubakaji wa demokrasia.. Itakuwa ni mchezo wa CCM kujitwalia rasilimali za taifa hili kwa wachache! Ikibidi hata jeshi liingilie kati kuhakikisha demokrasia inarudi... Hatuna shida na hili,kama tutatawaliwa na jeshi kuliko CCM isiyopenda demokrasia
 
Ushauri Zanzibar wakatae kupiga kura hadi iwepo tume huru
 
Binafsi siamini kilichotokea zanzibar,naona kama ndoto vile,je kuna wataalamu wa historia ambao wanaweza nambia nchi yeyote duniani ambayo imewahi kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu tofauti na nchi ya zanzibar?

mi nafikiri hii nchi imexhaingia kwenye kitabu cha world genes../ maajabu ya dunia kwa huu uchaguzi na matokeo yake
 
Back
Top Bottom