okonkwo jr
JF-Expert Member
- Jun 14, 2015
- 2,419
- 1,738
Historia inatujulisha kuwa uchaguzi wa February 1986 wa nchini Phillipines ulifutwa baada ya shinikizo toka nchi za nje pamoja na wananchi na viongozi wa jeshi la nchi yao baada ya Rais Marcos kuonekana dhahiri ameshinda kiti cha Rais kwa kuchakachua takwimu. Baada ya kufutwa matokeo hayo mshindi wa pili Corazon Aquino alitangazwa ndiye mshindi wa kiti cha Rais.
Vile vile historia inatueleza kuwa baada ya kubaini kuwa uchaguzi hautakuwa wa huru na wa haki walisusia kwenda kupiga kura. Mwaka 1983 asilimia 97.3 (97.3 %) ya wananchi wa Jamaica walisusia kwenda kupiga kura na tume iliona aibu kutangaza matokeo yatokanayo na 2.7 % ya wapiga kura. Mwaka 1997 asilimia 90.5 (90.5 %) ya wananchi wa Slovak walisusia kwenda kupiga kura na tume iliona aibu kutangaza matokeo yatokanayo na 9.5 % ya wapiga kura.
Refer: https://en.wikipedia.org/wiki/Philippine_presidential_election,_1986
Refer:https://en.wikipedia.org/wiki/Election_boycott
Binafsi siamini kilichotokea zanzibar,naona kama ndoto vile,je kuna wataalamu wa historia ambao wanaweza nambia nchi yeyote duniani ambayo imewahi kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu tofauti na nchi ya zanzibar?