anderson mbonika
Senior Member
- Feb 28, 2017
- 112
- 56
KILIMO NI MWALI HAJAREMBESHWA
Tanzania imebarikiwa sana kwa biashara ya kilimo. Hebu tizama hii:
1. Imezungukwa na nchi nane sugu kwa njaa
2. In maziwa makubwa kama Victoria, Nyasa, Tanganyika
3. Ina mito mikubwa kama Rufiji, Rufu, Malagarasi, Ruaha
4. Ina ekari takribani milioni 44 zinazofaa kwa kilimo lakini zinazotumika ni asilimia 23 tu
5. Ina soko kubwa la ndani takribani watu milioni 55
6. Ina ardhi na hali ya hewa inayoruhusu mazao yote ya tropiki na baridi kali
7. Ina mifugo ya kutosha kuzalisha mboji - Tanzania ni ya tatu Afrika kwa mifugo baada ya Ethiopia na Sudan
8. Ina wataalamu lukuki wa Kilimo pamoja na Chuo Kikuu mahsusi kwa kilimo
9. Ina vituo vya utafiti vya Kilimo maarufu kama Lyamungo, Uyole, Ukiliguru, Illonga, KATRIN, Maruku
10. Ina mabwana shamba wengi kushinda nchi zote za Afrika kutokana na sera ya awamu ya kwanza ya kujenga vyuo vya kilimo kila mkoa
11. Ina madini kibao ya kuweza kuzalisha mbolea kama phosphate, mbolea ya chumvichumvi, na Potassium (NPK).
Lakini Tanzania bado inaagiza bidhaa za kilimo toka nje!
Tatizo?
Ukisoma maandiko ya watafiti wetu na maprofesa wetu wanadai kuna sababu kama ubovu wa miundombinu, kukosekana masoko ya uhakika, kukosekana viwanda vya kusindika, ushiriki mdogo wa sekta binafsi, kukosekana malighafi za kilimo au bei kuwa juu, kukosekana mitambo ya mechanization, etc.
Hata KILIMO KWANZA imerudia hayohayo!
Ni vyema tukaelewa kuwa hata nchi za wenzetu walianza na kilimo lakini kikadorora mno! Mfano ni nchi kama Sweden, germany, Ireland, Italy, US, UK. Kilimo kilidorora kwa sababu mbalimbali: Kwa mfano kukua kwa miji ambako kulitwaa ardhi, kuibuka kwa sekta mpya kama utalii na viwanda n.k. ndio maana kwa mfano Ulaya vyama vya wafanyakazi wa sekta ya Kilimo vililazimika kufa au kujiunga na vyama vya sekta nyingine ili kujinusuru.
Lakini kubwa kabisa kilichofanya sekta ya kilimo idorore ni kupoteza mvuato kwa vijana!
Baada ya miji kama Stockholm, Copenhagen, Dublin na mingineyo kukua na kuwa na huduma za uhakika kama umeme, maji, usafiri, makazi, n.k. vijana hawakukubali tena kubaki mashambani kwenye vumbi, makazi duni na huduma hafifu za kijamii. Wakahamia mijini ambako kuna huduma zinazoendana na ndoto zao. Matokeo yake kilimo kiachukua umbo jipya. badala ya kuwa cha watu masikini (small scale) kikageuka kuwa cha watu matajiri (large scale). Ni kwa jinsi hii wenzetu wa US, Ulaya, Australia, China na India wameweza kudumisha kilimo chao. Ni nchi chache kama Japan ndio zimeweza kudumu na small scale kutokana na ufinyu wa ardhi. japan hakuna tofauti kubwa sana ya huduma baina ya 'vijiji' na 'miji'.
Kwa hiyo kama kweli Tanzania inataka kunufaika na kilimo lazima watu wakae chini wafikirie haya mawili:
1. Namna ya 'kurembesha' kilimo ili kiweze kuwavutia vijana. Vijana wa sasa wanataka waishi sehemu kuna maji, simu, mtandao, usafiri wa uhakika, umeme, hospitali, shule, vyuo, n.k. Hawawezi kwenda kulima Namtumbo au Uru Kishumundu au sehemu kama hiyo ambapo mawasiliano ni kwa barua ya posta, mwanga ni wa tochi, usafiri ni baisikeli! Yanawezwa kutengwa maeneo ya kilimo na kuwekewa huduma zote wapendazo vijana. Watakwenda kulima kwa wingi kama wanajua jioni wakishatoka shamba watapiga porojo facebook! Wakiwa wanaamia ndege shambani wataweza kwenda na feroza au kutuma meseji aletewe maji ya kunywa baridi! Tutajidanganya sana kuamini vijana wataenda kulima bila kuwatimizia mahitaji yao ya ujana. We must 'modernize and youthnize' our agriculture ama sivyo KILIMO KWANZA kitakuwa cha wazee wachovu!
2. Namna ya kurejea sera ya Mwalimu ya mashamba makubwa (large scale farming). Mashamba hayo yanaweza kuwa ya taifa au ya watu binafsi au vikundi vya vijana lakini wawe watanzania si wageni. Kuna mazao yanahitaji sana 'economy of scale'. Yaani kuna mazao faida inapatikana tu pale yanapolimwa eneo kubwa. Ndio yanalipa! Ni mazao ya thamani kubwa (high value crops) kama bangi, pilipili, mbaazi, choroko, dengu na maua pekee ndio yanafaa vishamba vidogovidogo. Mazao kama mpunga, ngano, shairi ukilima kishamba kidogo hailipi! Ni kwa kula nyumbani kwako tu! Utabaki masikini milele.
3. Jinsi ya ku industrialize kilimo ili tusiuze malighafi bali agric products. katika ari hii mpya ya kujenga viwanda basi tutoe kipaumbele kwa viwanda vidogo na vikubwa vya kuchakata mazao ya kilimo. Tusikimbilie kujenga viwanda ambavyio hatuna 'comperative advantage'! Sie advantage yetu ni kwenye kilimo. Tudhamirie kuifanya Tanzania 'an industrial agricultural country in Sub Saharan Africa'. Yaani mtu popote alipo duniani akifikiria kuhusu nguo, nyama, jibini, mchele, unga ngano, sembe, tomato sauce, juisi, n.k. akumbuke TANZANIA.
Kwa mfano hatuna advantage kwenye kutengeneza computer na simu hii wanayo DRC!
Hata kwenye chuma cha mchuchuma industrialization ilenge viwanda vya kuzalisha zana za kilimo kama matrekta, combine harvesters, seed drillers, majembe ya kukotwa na trekta, power tillers, malori, tailers, n.k. Tunaweza kuwapita wajerumani kuzalisha zana za kilimo na ku mechanize kilimo chetu na ziada tukauza Afrika nzima! Tutakuwa tumejenga viwanda sahihi kama tutajenga viwanda vya ku modernize kilimo chetu na ku process madini yetu.
Ndio maana Stigeler's Gorge ni mradi muhimu sana kwa Tanzania. Wanaopinga ni aidha hawajui au wanatumiwa! Ku modernize agriculture tunahitaji mno umeme wa uhakika. Umeme usiokonyezakonyeza au kuzimiazimia! Wanaodai utaharibu mazingira ni wale wanamazingira wanaojulikana kama 'preservanists' na si 'conservanists'! preservanists ni wana mazingira wasiojua dhana ya kuhifadhi mazingira. Waropokaji!
Conservanists ni wale wanaoamini lazima mazingira yabadilike ili maendeleo yapatikane. Huwezi kuwapa kipaumbele kima, buibui, chura, vipepeo, simba, nyumbu, fisi au mbweha ukaacha kuwapa kipaumbele wanadamu! Pale ambapo mahitaji ya binadamu yanahitajika viumbe wengine wote wanapewa siti ya nyuma! Hii haimaanishi kuwa wakati wa kutekeleza mradi wa Stiglers EIA isifanyike. La hasha. Ifanyike lakini hata ikidai vyura wengi na ndege adimu wataathirika isituzuie wanadamu kupata maendeleo. Zitafutwe mbinu za kupunguza madhara kwa ndege na vyura maana zipo! Mradi utekelezwe!
Binafsi kama mtaalamu niliwahi kushiriki tathmini ya mradi wa bomba la mafuta la misitu ya Urubamba nchini Peru. Mradi huu ulikuwa chini ya kampuni ya SHELL. Zilipigwa kelele na ma conservanists toka sehemu mbalimbali duniani ikabidi Smithsonian Institute itume timu ya wataalamu kwenda kufanya independent EIA.
Ni kweli misitu ya Urubamba ilikuwa na 'endemic species' nyingi za miti, ndege na vipepeo. Ni kweli vingeathirika kwa kuipishwa bomba la mafuta. lakini ni kweli pia bomba la mafuta lilikuwa na faida kubwa sana kwa nchi ya Peru! Ikaonekana ni kichekesho kulinda vipepeo na ndege na kuacha nchi haina mafuta! Mradi ulitekelezwa na ni miaka takribani 20 sasa watu wananufaika na mafuta na kina vipepeo na ndege ambao wakazi hawakunufaika na chochote wakahimishiwa misitu mingine! Lakini baadae ilikuja fahamika kuwa wafadhili wakubwa wa kampeni ya kupinga bomba ni wakulima wa coca! wazungu wa unga! Waliigeuza misitu himaya yao! hawakutaka watu wengine waende!
Inafanana fanana na wanaopinga Stieglers Gorge project! Nyuma ya pazia wapo wanaonufaika na kutokuwepo na Stieglers Gorge power generation! Wapuuzeni!
IT CAN BE DONE PLAY YOUR PART