Wataalamu wa magari msaada wenu tafadhali

Wataalamu wa magari msaada wenu tafadhali

cleokippo

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2014
Posts
2,118
Reaction score
1,797
Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza

nimenunua ki Gari fulani hivi bibayabaya ambacho kinaweza kunitoa sehemu moja kwenda nyingine

kihistoria mimi sijawahi kumiliki gar hata mwaka mmoja na hii ndio gari yangu ya kwanza aina ya starlet

Gari hii nimenunua kwa mtu hapa Mwanza, na tangu niinunue haijawachi kuniharibikia kabisa

Sasa nafikiria kusafir kwenda Dar hivyo nikapata wazo la kwenda na haka ka Gari no matter kwamba ni kabaya na sijawahi kisafiri nacho umbali mrefu

kilivyo hapa kwa hivi sasa kina tyre zote mpya, nimemwaga oil na kuweka oil mpya, majo yapo ya kutosha, wese lipo na kuna cash ipo mfukoni endapo litakata, mfumo wa umeme upo vzr kwamaana ya taa na endicator zote, break ipo vzr

sasa nauloza wataalam kuna kitu gani cha ziada ya kuangalia ili safari yangu iweze kuwa ya mafanikio?

sio mtaalam sana na ndio maana nimeingia jukwaani kuomba ushaur maana kwenye gari ninachojua mimi ni kuendesha tu bas

kwaiyo kitu gani tena muhimu natakiwa kuangalia ili nisikwame njiani?

Aksanteni
 
Ngoja wache wataalamu ila hujatuambia ni no gani ako ka stalet
 
Endesha gari hiyo tena kibati acha uoga , Starlet gari bhana… kwanza unaidhalilisha unaposema kibaya kibaya !! Hv unajua bei ya ENGINE yake complete??
 
Back
Top Bottom