Habari wana jf hususani wataalam ndani ya jukwaa hili. Kusema kweli nimekuwa nikisikia tu hili neno likitajwa( affidavit), lakini sijabahatika kupata ufafanuzi wa kina kwamba ni kitu gani? Kinatumika wapi na ukomo wake ni upi? Kwa minajili ipi hasa?. Nimeuliza hivyo kwa sababu kuna mtumishi mwenzangu ana likizo ya malipo Mwezi ujao ana cheti cha kuzaliwa mtoto wake lakini hajafunga ndoa na mkewe(hana cheti cha ndoa) but aliniomba nimsindikize mahakamani akapate affidavit kama supporting document ya kwamba ameoa pamoja na uthibitisho wa mtegemezi wake ili aambatanishe kwenye maombi ya fedha ya likizo. Je kuna uwezekano wa kitu kama hicho? Naomba wataalamu mnieleweshe
N.B jamaa yangu ni mtumishi serikalini kada ya afya
N.B jamaa yangu ni mtumishi serikalini kada ya afya