Iko vizuri sana ina nguvu kwenye milima,zingatia service.Baada ya mafuta kupanda bei mara dufu, nimeamua kuuza Brevis yangu kwa mil 6 kwani ilikuwa inakunywa sana mafuta.
Nimeamua ninunue pikipiki na chaguo langu ni Kinglion. Sina uzoefu sana na pikipiki japokuwa naweza kuendesha. Hivyo naomba wataalamu kesho naenda kununua mnielekeze mambo ya kuzingatia ili mwanajf mwenzenu nisijepigwa. Tafadhali karibuni kwa ushauri
Brevis haili mafutaBaada ya mafuta kupanda bei mara dufu, nimeamua kuuza Brevis yangu kwa mil 6 kwani ilikuwa inakunywa sana mafuta.
Nimeamua ninunue pikipiki na chaguo langu ni Kinglion. Sina uzoefu sana na pikipiki japokuwa naweza kuendesha. Hivyo naomba wataalamu kesho naenda kununua mnielekeze mambo ya kuzingatia ili mwanajf mwenzenu nisijepigwa. Tafadhali karibuni kwa ushauri
2400cc vs 5.7l petrolCc 2400 vs cc 150
SupportDah, sikupangii matumizi ya hela yako bro ila nafikiri ni vyema hiyo pesa uliyoipata ukaipasua mil 4 ukabaki na 2...
Hiyo 4 ukalenga ukachukua gari yenye cc ndogo kama vits, suzuki kei,zile gari jamii ya terrios kid/daihatsu ..
Kuna factor chache za kuconsider:
-kuna msimu wa masika
-kubeba mtu zaidi ya mmoja(familia)
-incase of accident pikipiki risk ya madhara ni kubwa zaidi
-ile watu kukusimamisha kwa kudhani wewe ni bodaboda its quite annoying
-psychologically utakuwa down ile transition kutoka brev hadi k-lion
NB: HIYO MILIONI 2 ILIYOBAKI NUNUA PILIPIKI UMPE KIJANA AFANYE BODA ILI IKULETEE MAFUTA YA HIYO VITS YAKO UTAKAYONUNUA
kakwambia anakaa mjini?labda anakaa mkoani,kijijini.Bora hata ungenunua Suzuki Kei yenye cc 600's ila siyo pikipiki aisee! Kiufupi utaboreka sana.
Imagine umepaki zako mjini, ukimsubiri wife afanye manunuzi, anakuja mdada na kukuuliza "eti kaka wewe ni bodaboda?" Aaaarghhhh!! π© Mara anakuja msela "oya boda nipeleke sehemu fulani!"
Hii ni nje ya dharau kutoka kwa wenye magari! Bado msimu wa masika haujaanza!!! Aisee ni kosa kubwa sana kuuza gari na kununua pikipiki! Hapo bado ajali! Maana mwili wako ndiyo hugeuka kuwa body!
By the way, Kinglion ni lipikipiki la kubebea mizigo mizito, na kupandia milima. Kama unanunua kwa ajili ya matembezi/kuendea kazini au mishe ndogo ndogo, ni bora ukanunua Haojue yenye cc 125.
We ndio hata mada hujaielewa, kasome tena na tena maana hiyo kichwa ni ngumu2400cc vs 5.7l petrol
Then which is which
Ni ujinga wa hali ya juu ku compare brevis na ractis, mara ist ..compare brevis na magari saizi yake eg Nissan fuga nk Kisha ndo uje useme brevis inakula mafuta