Watafuta vitu mnazingua sana jamani

Watafuta vitu mnazingua sana jamani

Matendo Andrew

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
748
Reaction score
367
Mitandao ya kijamii imekua suruhisho kwa watu wenye kujua kutumia Mimi mwenyewe nimekua nikinufaika nayo kwa kujifunza vitu mbalimbali kuuza na kununua vitu kwenye mitandao tofauti pamoja na huu wa JF.

Kinacho niboa unakuta mtu ametangaza kutafuta kitu fulani licha ya kuwa mbali mwingine anakua karibu lakini wanakua Kama wapuuzi hivi.

Yaani hawana userious Sasa wale wa Mikoani ndio kabisa mmoja alitangaza anataka kitu fulani nimempa picha nikimuulizia vipi unatuma mtu kukagua anasema eti mbona nina haraka sana khaaa!! Kumbe unataka kitu lakin hela huna au unataka kujua Bei ni Bora upost kuuliza utasaidiwa kuliko kusumbua watu.

Sometimes mtu anatumia mpaka gharama kuhakikisha unapata kitu kizuri lakini unakuta mnunuzi analeta vipengele.

HII IMENIKERA ACHENI BWANA
 
Kwani ni lazima aendane na muda wako mkuu? We cha msingi umeshamuonesha biashara yako basi relax.

Akiwa tayari atakuja mwenyewee, ukiona kimya jua hajaridhika na item yako.
 
Hata nami ninafanya biashara online, na hata hapa Jf nimekuwa nikitangaza biashara na nimefanya biashara pia.
Kwanza usilalamike kuhusu gharama unazo tumia kwasababu hiyo ndio maana halisi ya neno mtaji.
Na unapo fanya ama kutangaza biashara yako zingatia sana kauli njema kwa wateja wako, pia uvumikivu na subra ni kitu cha muhimu sana kwenye biashara.
Alafu......
Ebu punguza malalamiko mkuu, kwasababu sio kila mteja anapo kuulizia bidhaa basi lazima ainunuwe. Jaribu kuwa flexible hasa linapo kuja swala la biashara za online na umbali.
Na, ukome kuwatukana wateja wa mikoani pasipo sababu ya msingi, kwasababu sio lazima waridhike na bidhaa yako na haija andikwa sehem kwamba lazima wanunuwe kwako.
 
Siwezagi nunua kitu/Bidhaa yoyote kwa muuzaji kama mtoa post au wengine wote wanaofanana na wewe. Unapomwonyesha mteja bidhaa basi mwache akague kile yeye alichokuja ameamini juu ya bidhaa anayohitaji, Mpe kauli nzuri za uteja na kuomba kumsadie endapo atahitaji maelekezo, Mwaminise juu ya bidhaa husika na Mpe mda wa kufanya maamuzi. Na kama hajanunua bidhaa yako siku hiyo mshukuru na mkaribishe siku nyingine tena kama si yey basi jua atamwonyesha mwingine. Wema huwa haupotei.
 
Wengi ni madalali..pale unapotaka kukuiona kitu live ndio shughuli inaanzia hapo,anajajua ata kudirect kwa muuzaji halisi na gawio lake hatopata
 
Unaongeleaje kuhusu wauzaji fake?
Kuna madalali wengi humu ni fake, nitaanika uozo wao na utapeli humu siku moja
Mitandao ya kijamii imekua suruhisho kwa watu wenye kujua kutumia Mimi mwenyewe nimekua nikinufaika nayo kwa kujifunza vitu mbalimbali kuuza na kununua vitu kwenye mitandao tofauti pamoja na huu wa JF.

Kinacho niboa unakuta mtu ametangaza kutafuta kitu fulani licha ya kuwa mbali mwingine anakua karibu lakini wanakua Kama wapuuzi hivi.

Yaani hawana userious Sasa wale wa Mikoani ndio kabisa mmoja alitangaza anataka kitu fulani nimempa picha nikimuulizia vipi unatuma mtu kukagua anasema eti mbona nina haraka sana khaaa!! Kumbe unataka kitu lakin hela huna au unataka kujua Bei ni Bora upost kuuliza utasaidiwa kuliko kusumbua watu.

Sometimes mtu anatumia mpaka gharama kuhakikisha unapata kitu kizuri lakini unakuta mnunuzi analeta vipengele.

HII IMENIKERA ACHENI BWANA
 
Huyu ni aina ya madalali anbaye akipigiwa simu ya kutafta kitu yeye anagiza na BIA KRETI kwa bajeti ya kitu asichouza bado

Back
Top Bottom