Uchaguzi 2020 Watakaomwangusha vibaya Dkt. Magufuli ni wana CCM wanaojielewa

Uchaguzi 2020 Watakaomwangusha vibaya Dkt. Magufuli ni wana CCM wanaojielewa

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2020
Posts
275
Reaction score
802
Nipo kwenye makundi mengi ya WhatsApp ya CCM mikoa mitano. Ni dhahiri kwa hoja za Lissu ni hakika kuna miguno ya kuvumilia maumivu. Tofauti na matarajio ya wanaCCM wengi waliodhani hoja za miundombinu zingembeba Magufuli, la hasha, hoja za Lissu ndiyo mahitaji ya wananchi wengi.

Kutokana na ilani ya CCM kusheheni ndege, meli na reli, na kukosa ahadi zinazowagusa watanzania wengi, kumetokea sintofahamu ndani ya chama hiki ya kudandia hoja za Lissu ambazo hazipo kwenye ilani ya CCM.

Kwa mfano, hoja ya kuboresha maslahi ya watumishi haipo sehemu yeyote katika ilani ya chama chetu cha kijani. Lakini baada ya Lissu kuiongea Mara kwa mara kwa kuwa ipo kwenye ilani ya Chadema, Naye Magufuli ameidandia bila utaratibu na sasa inamtesa sio yeye tu bali na watetezi wake.

Hoja nyingine ambazo chama chetu kimedandia ni hoja ya Bima ya Afya kwa wote, kulipwa madeni yote kwa watumishi, mikopo kwa wanafunzi, TRA na wafanyabiashara, nk.

Hivi karibuni Bashiru aliwaamuru vijana wa CCM wajibu hoja za wapinzani haraka. Hahaha!!. Nipo kwenye makundi manne ya wasomi wa vyuo vikuu, yaani shirikisho la vyuo vikuu, kuna mjadala mzito kuwa hoja za Lissu hazijibiki kwa kuwa anayoahidi ndiyo hasa mahitaji ya jamii. Kundi moja likaenda mbele zaidi na kujadili kuwa kukosekana kwa mikopo kwa wanachuo wa vyuo vikuu ni kero ambayo inakiangusha CCM kwa vijana wa vyuo vikuu.

Ndugu zangu mwanaccm wanaojielewa, naomba nishauri ila najua ushauri wangu hautakubalika kwa kuwa mwenye akili ndani ya chama chetu ni Magufuli peke yake. Nashauri tuipitie ilani yetu iliyosheheni miundimbinu, tuweke mambo yanayowagusa wananchi wa kada nyingi hususani vijana.

Naomba kuwasilisha

Ajira elfu 13 za walimu hoyeee
 
pambaneni na hali yenu. Naona wagombea wenu washaanza kujitoa
Ndo aina ya wanaccm walioambiwa wajibu hoja haraka ndo kama huyu. Na hapa ndio ameshajibu hoja! CCM ina kazi. Imebeba vijana mizigo wasiojielewa, mazungumzo yao ni kusaka uteuzi. Amkeni CCM wenzangu.
 
"Vijana wa CCM mjibu hoja za upinzani haraka"- Bashiru
 
pambaneni na hali yenu....Naona wagombea wenu washaanza kujitoa
Naona magufuli wenu ameshindwa kuomba kura sasa anatoa vitisho!!! Mwambie kwa vitisho tu vya jana na juzi ajue kuwa kile ni kiashiria kimojawapo cha uchaguzi kutokuwepo huru na wa haki!
 
Magufuli hawezi hata kunadi sera anatoa vitisho tu.
Hii ni aibu, yeye anajiona rais, akiwaona walinzi mpaka juu ya miti anajua ameshashinda. Magufuli unahitajika kusaka kura kwa wapiga kura karibia milioni 20
 
Back
Top Bottom