Watakaopata Division IV Kutosoma Mafunzo ya Ualimu

Watakaopata Division IV Kutosoma Mafunzo ya Ualimu

tatanyengo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2011
Posts
1,133
Reaction score
280
Serikali ina mpango wa kufuta ufaulu wa Daraja la IV (Division IV) kwa wahitimu wa kidato cha IV kwenda kusoma katika vyuo vya ualimu. Suala hilo limedokezwa leo na Naibu waziri -Phillipo Mulugo alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na mbunge wa Longido bungeni Dodoma.

Mulugo amesema wameanza kwa kuondoa point 28 na wataendelea kufanya hivyo lengo likiwa kufuta kabisa waliopata Division IV kusomea ualimu.

My take: Division IV ndiyo ushindi kwa watoto wetu wanaosoma katika shule zetu hasa za Kata sasa wakitupwa nje ya ulingo huu litakuwa ni janga la kitaifa.

Binafsi pia sidhani kama kuwachukua walipata division I, II, na III ndiyo kigezo pekee cha kuboresha elimu nchini -serikali iboreshe mazingira kwa walimu na matokeo watayaona!
 
Ni sawa..ila hao div 4 watakuwa wanawatupa wapi sasa?
 
ni sawa lkn wawatafutie ajira mbadala.
Hii itatoa changamoto ya wanafunzi kujitahidi zaidi kwani kuna wanaosoma shule za kata na wanafaulu vzr tu.
Hata serekali isingefuta automatic zingejifuta zenyewe baada ya muda kutokana na ushindani.
 
N njia bora ya kuondoa wazembe wa 25,24,23. Wakawe walimu kwa upande mwingine ilo kundi la iv litakwenda wap labd jeshin
 
kilimo kwanza+ shule za kata+migomo+ugumu wa maisha=hatima ya uchaguzi 2015
 
Wanampango wa kuchukua wenye 0 kuwa walimu
 
cbe,ifm wanahtaj D 3 tu karbun st kayumba.
 
Back
Top Bottom