Watalaam wa kiroho naomba tafsiri ya jambo hili

Watalaam wa kiroho naomba tafsiri ya jambo hili

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,536
Reaction score
4,621
Hapo vipi

Kuna kitu cha ajabu huwa kinanitokea kwa muda mrefu sasa, nikawa nachukulia kama jambo la kawaida ila sasa naona..sio jambo la kawaida kabisa.

Iko hivi kipindi nasoma kuanzia secondary mpaka university, nikichua daftari au paper kusoma mara mara japo sio kila siku inajitokeza kitu kama kinywele kinakaa pale kwenye daftari au paper ninayosoma kipindi cha nyuma ilikuwa nachukulia kama jambo la kawaida ila sasa naona nilichunguze kwa undani zaidi kama ni kawaida au la.

Kwa sasa hali hii nimeanza kuona mara kwa mara kwenye simu ninayotumia. Nikiwa nafanya mambo yangu kile kinywele kinajitokeza juu ya screen ya simu najiuliza kinatoka wapi na kwanini kinajitokeza katika mazingira kama haya.

Naombeni ushauri juu ya hili kwasababu limeanza kuniumiza kichwa, hichi nini.
 
Tafsiri yake hapo hiko kinywele kinaashiria kuna mtu kakuchukulia nyota sasa iyo ni ishara inayokuonesha sasa kwa ushauri jaribu kwenda kwa viongozi wa dini haraka sana yani narudia nenda haraka sana.
 
Tafsiri yake hapo hiko kinywele kinaashiria kuna mtu kakuchukulia nyota sasa iyo ni ishara inayokuonesha sasa kwa ushauri jaribu kwenda kwa viongozi wa dini haraka sana yani narudia nenda haraka sana
Dah!! Hii issue nimeipuuzia muda mrefu kumbe ni jambo la hatari sana..asante kwa ushauri
 
Tafsiri yake hapo hiko kinywele kinaashiria kuna mtu kakuchukulia nyota sasa iyo ni ishara inayokuonesha sasa kwa ushauri jaribu kwenda kwa viongozi wa dini haraka sana yani narudia nenda haraka sana
Viongozi wa dini wapi mkuu kina gwajima na mwamposa?
 
Hizo ni dalili za jini mbaya sana ila ntakusaidia mjukuu wangu. Tuma nauli nikufuate ulipo nikupe tiba. Ukizembea hali itakuwa mbaya zaidi.
Ni kweli hili ni tatizo ila naona wewe unataka kunipiga hela tu. Mzee hapa naumia acha masihara
 
Ni kweli hili ni tatizo ila naona wewe unataka kunipiga hela tu..mzee hapa naumia acha masihara
Nimewasaidia wengi sana mjukuu wangu, siwezi kulitumia tatizo lako kama chanzo cha hela. Ni msaada tu na kutoa ni kwa mtu aliojazika imani moyoni.
 
umeshawahi kukipangusa hicho kinywele hapo juu ya kioo cha simu au karatasi unayosoma? kinatoka?

nimeuliza maana isije kuwa ni kinywele tu cha nyusi kipo katika jicho lako na unakiona tu muda huo kwa vile unakuwa umeconcentrate ndo maana!
 
Kipindi cha nyuma ilikuwa na kipangusa then nakitoa nachukulia kawaida tu..ila imekuwa too much
 
Kuna dalili ya kuokota TANZANITE ya thamani ya TRILLION 7.8..
Kapige surulu mzee..

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Back
Top Bottom