papason
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 5,119
- 5,698
Marekani na washirika wake pamoja na kutumia takribani dola bilioni 89 ($89 billions) kwa kuvifundisha na kuvipa silaha vikosi vya jeshi la Afghanistan kwa takribani miaka 20 hivi, iliwachukua mwezi mmoja tuu kwa Taliban kuvi fyekelea mbali na kuvisambaratisha vikosi vya jeshi la Afghanistan baada ya ‘washirika wao’ kutangaza kuviondoa vikosi vyao nchini Afghanistan.
‘‘Allahu Akbar’ wapiganaji wetu wamefanikiwa kuichukua ikulu huku serikali dhalimu ikianguka, kibaraka mkuu ( raisi Ashraf Ghani ) na vikosi vyake wamekimbia na sasa vita imekwisha.!
’ haya maneno ya msemaji wa Wa -Taleban Suhail Shaheen na kuwaasa wakazi wa Kabul hawana haja ya kuwa na wasiwasi na kwamba mali na maisha yao ni salama. "Sisi ni watumishi wa watu na wa nchi hii,"
Taliban imetangaza ushindi nchini Afghanistan baada ya kuteka mji mkuu Kabul, na kutamatisha karibu miaka 20 uwepo wa Marekani na washirika wake nchini humo
Kutokea Kandahar ( kusini mwa nchi) adi Mazar-i-Sharif ( kaskazini), Herat ( Magharibi) mpaka Jalalabad ( mashariki) huku Kabul ukiwa mji mkuu wa mwisho nchini Afghanistan kudhibitiwa na Taliban, baada ya wapiganaji wake kuikamata miji zaidi ya miji kumi kwa muda wa siku kumi tuu. Aliye kuwa raisi, Ashraf Ghani, alitimua mbio na kukimbilia Tashkent katika nchi jirani ya Uzbekistan
Kikubwa zaidi kwa takriban masaa 36 tangu wa Taleban wauteke mji wa Kabul, hakuna raia au mwananjeshi yeyote aliye uwawa au kuchinjwa tofauti kabisa na ilivyo kuwa ikielezwa apo kabla na Marekani na washirika wake kuwa watu wengi watauwaa na kuchinjwa pindi Wa Taleban watakapo ingia Kabul....
Kongole kwa Wa Taleban kwa kuweza kuidhibiti tena nchi walionyang'anywa na wavamizi takribani miaka 20 iliyo pita,