Watalii, Wawekezaji, na Miradi Vyote Juu

Watalii, Wawekezaji, na Miradi Vyote Juu

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Hizo ndio Kauli nazisikia wadau wakiniambia....

Mapato, na Mikopo navyo tunapata, yaani mambo yapo sawa sawia...

LAKINI najiuliza hizo Pesa zote za hao watalii, mikopo na Tozo tunazopata kwanini sioni maendeleo kitaa sambamba na hizo neema tunazopata ?

Ni wapi panavuja ? Kama Royal Tour tumepata watalii lukuki ambao hapo nyuma hatukuwapata. Hizo chenji za ziada zinakwenda / zimekwenda wapi ?
 
Ungeongeza na Njaa Juu.
Royal tour haipimiki. Haina takwimu za Uhakika wala kisayansi kupewa upeo wowote ule wa juu.
 
Ungeongeza na Njaa Juu.
Royal tour haipimiki. Haina takwimu za Uhakika wala kisayansi kupewa upeo wowote ule wa juu.
Tunaambiwa Utalii umeongezeka maradufu..., Ni Vema na Haki, ila sijui kwanini hatuulizi hilo Ongezeko linafanya nini, mbona kukopa na Tozo ambazo zilikuwa hazipo nazo zimeongezeka ?
 
Hizo ndio Kauli nazisikia wadau wakiniambia....

Mapato, na Mikopo navyo tunapata, yaani mambo yapo sawa sawia...

LAKINI najiuliza hizo Pesa zote za hao watalii, mikopo na Tozo tunazopata kwanini sioni maendeleo kitaa sambamba na hizo neema tunazopata ?

Ni wapi panavuja ? Kama Royal Tour tumepata watalii lukuki ambao hapo nyuma hatukuwapata. Hizo chenji za ziada zinakwenda / zimekwenda wapi ?
Mama Samia! Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Please ikikupendeza watanzania wako wengi wanauwezo, wabunifu na wanamaono ! Fanya nao kazi sio lazima wawe ccm! Ni watanzania pia na wataifanyia nchi yao makubwa!
Basi mteue Kimei ashike hiyo wizara ya fedha!
 
Tunaambiwa Utalii umeongezeka maradufu..., Ni Vema na Haki, ila sijui kwanini hatuulizi hilo Ongezeko linafanya nini, mbona kukopa na Tozo ambazo zilikuwa hazipo nazo zimeongezeka ?
Ni ilani ya CHI CHi Emu
Walituambia COVID-19 iliongeza ukoko kama sio ukakasi wa Watalii kutokuja, wengine walidiriki kusema ati ni kwa sababu ya sera mbovu (zao wenyewe zinazoitwa ilani) Juu ya COVID-19 ndio maana utalii ulishuka...wamebadilisha gia angani...

Lakini, naweza kusema kuwa, ni vizuri ilivyotokea hivyo, kwani Serikali imejifunza kutokuwa wategemezi- kuwa haziwezi kulala na kufikiria kuwa vyanzo vya vipato vya nchi au Serikali, ni fedha za kigeni tuu kwa mfano hapa kwetu karibia asilimia kubwa ya mapato ya fedha za kigeni zilitoka kwenye Utalii. Uviko ulivyotukumba mabakuli yalipungua

. Hilo la tozo na sijui vikolokolo gani vinahitaji ubunifu wa hali ya juu na sio kuona kila kita kinachong'aa ni dhahabu, nikimaanisha sio kila eneo linalonyesha mzunguko mzuri wa hela lipigwe tozo! Wanajifunza. Tunajifunza, tutafika.

Wangeanza tozo kwenye V8, pamoja na wawekezaji uchwara kama vile mama ntilie wanaotoka Nje(mfano tu). tsk tsk
 
Binafsi naona ni Usanii na Propaganda tu....

Yaani siku hizi kuwekeza kwenye Propaganda ndio formula (Danganya wananchi piga pesa kwa faida yako na ndugu zako shida zitakazokuja mbeleni shauri yake atakayekuwepo kipindi hicho)..., Huku wananchi tuliopigwa propaganda tutaendelea kupigwa propaganda kwamba makosa sio ya wa sasa bali aliyepita....

Ingawa shida kubwa matatizo yatoka from BAD - WORSE to WORST
 
Back
Top Bottom