Watambue Iranic People - Iranian People (Uwezo wao) - Siyo War

Watambue Iranic People - Iranian People (Uwezo wao) - Siyo War

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Leo katika mwendelezo wa kuchambua na kuijua Iran kiundani zaidi ni muhimu kuwatambua hawa watu ni wa aina gani na asili yao ni wapi.

Waajemi
Neno waajemi ni neno la kiswahili lilitoholewa kutoka kwenye lugha ya kiaarabu al-'ajam ikiwa na maana ya watu wasioweza kuzungumza kiarabu neno la kiarabu (Ajam) likiwa na maana ya mute.

Katika kusambaa kwa utamaduni wa waarabu waliwaita watu wasioweza kuongea lugha ya kiarabu kuwa ni Al-'ajam. Kwakuwa kiswahili kilianza kuzungumzwa pwani ya Tanzania na watawala wa eneo hilo walikuwa ni waarabu kutoka omani waliwaita watu kutoka "Persia" kuwa ni Al-'ajam. Wengi walitoka katika eneo linaloitwa "Shiraz". Na hawa washirazi waliungana na Waafrika akitika kupinga unyonyaji wa waarabu. Huko zanzibar walianzisha chama cha siasa kinachoitwa Afro-Shiraz Party (ASP)

Neno Persia
Kuna mji mmoja huko Iran ulikuwa unaitwa Persia, lakini wagriki waliwaita watu wote waliotoka huko ni Persia. Kutokana na hitoria ya maeneo mengi kuandikwa na wagriki utawala huo (Kutoka Western world) uliitwa Persian Empire.

Greece refers to all of Iran and its subjects as Persia.

Je, Warani walitokana na Makabila Yapi?

Watu wa Irani waliibuka katika millennium ya kwanza BC. Makabila yaliyowahusisha wa Iran ni:-

  1. Alans
  2. Bactria
  3. Dahae
  4. Khwarazm
  5. Massagetae
  6. Medes
  7. Parthians
  8. Sagartians
  9. Sakas
  10. Sarmatians (Wasamalia kwenye Biblia)
  11. Scythians
  12. Sogdians
  13. Cimmerians
Hao hapo juu ndio Wairan kwa asili.

Je, Kwa Sasa Wairan ni Akina nani?
Wairan sio wale tu wanaoishi katika nchi ya Iran. Bali wairan ni pamoja na:-

  1. Baloch (Hawa wapo Iran, Pakistan na Afghanistan)
  2. Gilaks (Hawa wapo kusini mwa Caspian Sea)
  3. Kurds (Hawa wapo Uturuki, Iraq, Syria na Iran)
  4. Lurs (Hawa wapo Magharibi mwa Iran)
  5. Mazanderanis(Hawa wapo Maeneo ya Caspian Sea)
  6. Ossetians (Hawa wapo kwa wingi Russia na Georgia)
  7. Pamiris (Wapo kwa wingi Tajikistan, Afghanistan, Pakistan na China)
  8. Pashtuns (Wapo kwa wingi, Pakistan, Afghanistan na India)
  9. Tats (Wapo kwa wingi Azerbaijan na Russia)
  10. Tajiks (Wapo kwa wingi Afghanistan, Tajikistan na Uzbekistan)
  11. Talysh (Wapo kwa wingi Azerbaijan na Iran)
  12. Wakhi (Wapo kwa wingi Afghanistan, Tajikistan, Pakistan na China)
Nitaendelea .......
 
Ni watu wenye akili sana sijui waliingiaje huo mkenge wa dini ya mwarabu, imewalemaza sana, wangekua supapawa leo hii.
Nilisoma sehemu wananchi wengi Iran wanaomba kama vipi hayo mayatollah yapigwe mabomu nchi ifunguke.

Wamejaza haya mabango kote, wanaomba uongozi wao wale waze wavaa dera wapigwe.

GLVpC4vbwAAFYd0.jpg
 
Ni watu wenye akili sana sijui waliingiaje huo mkenge wa dini ya mwarabu, imewalemaza sana, wangekua supapawa leo hii.
Nilisoma sehemu wananchi wengi Iran wanaomba kama vipi hayo mayatollah yapigwe mabomu nchi ifunguke.

Wamejaza haya mabango kote, wanaomba uongozi wao wale waze wavaa dera wapigwe.

GLVpC4vbwAAFYd0.jpg
mayatoula komenei hayajawai kuwa na akili
 
NENO IRAN
Neno Iran limetokana na neno Arya au ariya likiwa na maana ya skillfully.
Baada ya Islamic kuweza kulitawala eneo waarabu waliita Eran (of the Aryas).
Hii ndilo eneo wanalokaa Baloch (Iranian)
1713365174751.png
 
MAPINDUZI YA IRAN NA LENGO LAKE
Ukitaka kuyajua mapinduzi ya Iran unatakiwa kumuelewa Ruhollah Khomeini. Yeye alikuwa ni mwanazuoni aliyekuwa akifundisha masuala ya Falsafa ya Siasa na Dini.
Mwanazuoni huyu alikuwa akifundisha dini ya kislam(Shia). Alisoma ancient Greek philosophy na alivutiwa sana na Aristotle.
1713370654099.png

Mapinduzi ya Iran hayakuanza ghafla. Yalianza kwa awamu. Na lengo la mapinduzi ya Iran yalikuwa:-

  1. Kupinga utawala wa Kifalme
  2. Kupinga Siasa za West and East
  3. Kueneza dini ya Shia kama msingi wa Uislam
  4. Kuondoa Utawala wa Wazayuni
BAADA YA MAPINDUZI
Baada ya mapinduzi 1979 Nchi za Kislam zilizokuwa zinaogozwa Kifalme zilijawa na wasiwasi kuwa zinaweza kupinduliwa.
Nchi kama Saudia Arabia ndiyo ilikuwa na wasiwasi mkubwa.
Kwakuwa Siasa za Iran zilibadilika na kuwa hazifungamani na upande wowote USA na USSR zilikata uhusiano na Iran.
Ulaya na Marekani zilianza kuipiga sanction Iran. Huku nchi za kislam zikiitenga.
Saddam Hussein wa Iraq (September 1980 to August 1988) aliona ndio nafasi yake ya kuweza kuivamia Iran ili aweze kuongeza eneo. Lakini Iran waliweza kumshinda Iraq. Saddam Hussein aliomba waweze ku sign makubaliano kusitisha vita. Lakini Ruhollah Khomeini alikataa kuwa anaitaka Iraq yote iwe Shia.
Tangu 1979 Iran ilikuwa katika uhusiano mbaya baina ya nchi za Ulaya, USA na USSR. Ni nchi ya Switzerland huko ulaya ndio walishirikiana nao. Na kwa karibu sana China, Pakistan na North Korea ndio walikuwa wakiipiga tafu.
BAADA YA KUANGUKA KWA USSR
Baada ya USSR kuanguka Urusi ilirejesha uhusiano na Iran. Huku Putin amekuja kuongeza uhusiano huo.
Kujiunga Shanghai Cooperation Organization
Iran ni Member wa nchi za mashirikiana SCO:

  1. China
  2. India
  3. Iran
  4. Kazakhstan
  5. Kyrgyzstan
  6. Pakistan
  7. Russia
  8. Tajikistan
  9. Uzbekistan

KUJIUNGA BRICS
Mwaka jana Iran imekuwa moja ya nchi zilizo katika umoja wa BRICS
1713371371620.png


UMOJA WA OPEC
Iran ipo katika umoja wa nchi zinazouza mafuta duniani.
1713371464996.png


Kulingana na alikotoka mpaka sasa. Iran inaendelea kujiimarisha na kuwa taifa imara zaidi.
 
Kwa asili hakuna watu wanaitwa waajemi.
 
Back
Top Bottom