Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
U NAFANYA unachokipenda? Basi una bahati sana.
Kuna mastaa wa soka unaweza kusema wanafanya wasichokipenda, kwa sababu wasipokuwa kwenye mechi, basi huwezi kuwakalisha chini mbele ya televisheni ili kutazama nao mechi pamoja.
Kuna baadhi ya wanasoka wanatamba kwenye mchezo huo kwa sababu tu imekuwa sehemu ya ajira inayowaingiza kipato, lakini si kwamba ni wanazi wa mchezo huo kihivyo. Yaani kama hawapo uwanjani kucheza, hawana muda wa kutazama mechi kupitia televisheni.
Mastaa hao hupata shida sana wanapokuwa chini ya kocha mwenye staili ya kutazama video za wapinzani ili kufahamu namna ya kuwakabili. Mastaa hawa hawangalii mechi za soka kupitia televisheni.
GARETH BALE
Supastaa wa Real Madrid na Wales. Aliweka rekodi ya dunia mwaka 2013 wakati aliponaswa na Los Blancos kutoka Tottenham Hotspur kwa ada ya Pauni 85 milioni. Si mwanasoka wa mchezomchezo, lakini utashangaa, staa huyo hapendi kutazama soka kwenye televisheni na aliwahi kusema hivi wakati alipoulizwa juu ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu yake ya Real Madrid na PSG, Bale alisema: “Huwa sipendi kabisa kuangalia mechi kwenye televisheni ni bora hata nitazame gofu.”
LIONEL MESSI
Mwanasoka bora katika kizazi chake na pengine kizazi kingine chochote kile kilichowahi kutokea kwenye mchezo wa soka. Lakini, kwa uhodari wake wote, Messi hapendi kutazama mechi ya soka kwenye televisheni na anapokaa mbele ya televisheni, basi anachokifanya ni kutazama katuni tu, kitu ambacho wakati mwingine kimekuwa kikimpa shida mkewe, mrembo Antonella. Messi alisema: “Siangalii mechi ya soka kwenye televisheni, Antonella huwa namkwaza sana. Napenda kutazama katuni na mwanangu Thiago.”
NEYMAR
Pengine supastaa huyo wa Kibrazili abadilike kwa sasa baada ya kufanya uhamisho unaoshikilia rekodi ya dunia wakati aliponaswa na PSG kutoka Barcelona kwa uhamisho wa Pauni 198 milioni. Lakini, kwa kipindi alichokuwa Barcelona, Neymar alisema hawezi kukaa chini na kutazama mechi kupitia televisheni, wakati mechi yenyewe ikiwa si ya Barcelona.
Alisema hivi: “Siwezi kuangalia mechi kama si ya Barcelona. Siwezi kutazama mechi za Real Madrid wala za timu nyingine yoyote ile.” Labda kwa sasa Neymar atakuwa anatazama mechi za PSG tu.
RONALDINHO
Hivi majuzi tu alitangaza kustaafu baada ya miaka kadhaa ya kuutendea haki mchezo huo. Mbrazili huyo aliyecheza soka la ubora mkubwa kabisa akitamba pia kwenye klabu kadhaa za Ulaya kuanzia PSG, Barcelona na AC Milan.
Lakini, kufanya vizuri kote huko, Ronaldinho hakuwa akihangaika kuzitazama timu nyingine zikicheza kwa sababu hakupenda kuangalia mechi ya soka kwenye televisheni na alisema: “Sipendi kutazama mechi, napenda kucheza. Siwezi kukaa mbele ya televisheni kwa dakika 90 kwa ajili ya kuangalia matukio tu.”
GABRIEL BATISTUTA
Muargentina huyo alikuwa mwanasoka tofauti na wengine wote unaweza kusema hivyo. Batistuta, aliyekuwa bonge la straika zama hizo, alitamba kwenye soka, lakini kitu cha ajabu alikuwa haupendi mchezo huo kuliko kawaida.
Kwa Batistuta ishu haikuwa tu hapendi kutazama mechi kupitia televisheni, bali mchezo wenyewe kwa ujumla kwani alipotoka kwenye mechi tu, hakutaka kabisa kusikia kitu kinachoitwa soka.
Anapokuwa nje ya uwanja, Batistuta hapendi kabisa mambo ya soka, yaani hana muda wa kupiga stori za mchezo huo.
Sent using Jamii Forums mobile app