Watambue wachezaji wasiopenda kuangalia mpira kwenye luninga

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
U NAFANYA unachokipenda? Basi una bahati sana.

Kuna mastaa wa soka unaweza kusema wanafanya wasichokipenda, kwa sababu wasipokuwa kwenye mechi, basi huwezi kuwakalisha chini mbele ya televisheni ili kutazama nao mechi pamoja.

Kuna baadhi ya wanasoka wanatamba kwenye mchezo huo kwa sababu tu imekuwa sehemu ya ajira inayowaingiza kipato, lakini si kwamba ni wanazi wa mchezo huo kihivyo. Yaani kama hawapo uwanjani kucheza, hawana muda wa kutazama mechi kupitia televisheni.

Mastaa hao hupata shida sana wanapokuwa chini ya kocha mwenye staili ya kutazama video za wapinzani ili kufahamu namna ya kuwakabili. Mastaa hawa hawangalii mechi za soka kupitia televisheni.

GARETH BALE
Supastaa wa Real Madrid na Wales. Aliweka rekodi ya dunia mwaka 2013 wakati aliponaswa na Los Blancos kutoka Tottenham Hotspur kwa ada ya Pauni 85 milioni. Si mwanasoka wa mchezomchezo, lakini utashangaa, staa huyo hapendi kutazama soka kwenye televisheni na aliwahi kusema hivi wakati alipoulizwa juu ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu yake ya Real Madrid na PSG, Bale alisema: “Huwa sipendi kabisa kuangalia mechi kwenye televisheni ni bora hata nitazame gofu.”

LIONEL MESSI
Mwanasoka bora katika kizazi chake na pengine kizazi kingine chochote kile kilichowahi kutokea kwenye mchezo wa soka. Lakini, kwa uhodari wake wote, Messi hapendi kutazama mechi ya soka kwenye televisheni na anapokaa mbele ya televisheni, basi anachokifanya ni kutazama katuni tu, kitu ambacho wakati mwingine kimekuwa kikimpa shida mkewe, mrembo Antonella. Messi alisema: “Siangalii mechi ya soka kwenye televisheni, Antonella huwa namkwaza sana. Napenda kutazama katuni na mwanangu Thiago.”

NEYMAR
Pengine supastaa huyo wa Kibrazili abadilike kwa sasa baada ya kufanya uhamisho unaoshikilia rekodi ya dunia wakati aliponaswa na PSG kutoka Barcelona kwa uhamisho wa Pauni 198 milioni. Lakini, kwa kipindi alichokuwa Barcelona, Neymar alisema hawezi kukaa chini na kutazama mechi kupitia televisheni, wakati mechi yenyewe ikiwa si ya Barcelona.

Alisema hivi: “Siwezi kuangalia mechi kama si ya Barcelona. Siwezi kutazama mechi za Real Madrid wala za timu nyingine yoyote ile.” Labda kwa sasa Neymar atakuwa anatazama mechi za PSG tu.

RONALDINHO
Hivi majuzi tu alitangaza kustaafu baada ya miaka kadhaa ya kuutendea haki mchezo huo. Mbrazili huyo aliyecheza soka la ubora mkubwa kabisa akitamba pia kwenye klabu kadhaa za Ulaya kuanzia PSG, Barcelona na AC Milan.
Lakini, kufanya vizuri kote huko, Ronaldinho hakuwa akihangaika kuzitazama timu nyingine zikicheza kwa sababu hakupenda kuangalia mechi ya soka kwenye televisheni na alisema: “Sipendi kutazama mechi, napenda kucheza. Siwezi kukaa mbele ya televisheni kwa dakika 90 kwa ajili ya kuangalia matukio tu.”

GABRIEL BATISTUTA
Muargentina huyo alikuwa mwanasoka tofauti na wengine wote unaweza kusema hivyo. Batistuta, aliyekuwa bonge la straika zama hizo, alitamba kwenye soka, lakini kitu cha ajabu alikuwa haupendi mchezo huo kuliko kawaida.
Kwa Batistuta ishu haikuwa tu hapendi kutazama mechi kupitia televisheni, bali mchezo wenyewe kwa ujumla kwani alipotoka kwenye mechi tu, hakutaka kabisa kusikia kitu kinachoitwa soka.
Anapokuwa nje ya uwanja, Batistuta hapendi kabisa mambo ya soka, yaani hana muda wa kupiga stori za mchezo huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majina yao tafadhali

The good, the bad and the ugly.
 
Alisema hivi: “Siwezi kuangalia mechi kama si ya Barcelona. Siwezi kutazama mechi za Real Madrid wala za timu nyingine yoyote ile.” Labda kwa sasa Neymar atakuwa anatazama mechi za PSG tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majina yao tafadhali

The good, the bad and the ugly.
 
Karibuni kuongezea kama kuna mahali nimesahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatatokea tena fundi wa mpira ulimwenguni like Messi...Messi ni kipaji kutoka kwa Mungu....na ndio maana hana ujinga wa kuangalia wachezaji wenzie wanavyocheza wakati yeye ni completed player kila idara, yeye ni mwalimu wa soka...so hahitaji funzo kutoka kwa wachezaji kama wachezaji... Imagine mchezaji kama huyu hakosekani katika vikosi bora kuwahi kutokea vinavyopangwa na makocha bora ulimwenguni, wachambuzi bora ulimwenguni na wachezaji wenyewe....lazima awepo in a squad...


Nipo kwenye utu uzima kwa sasa, wachezaji wangu bora kuwahi kutokea katika ulimwengu ni LEONEL MESSI AND YO SOL EL DIEGO ARMANDO MARADONA
 
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyojifunza mengi kutoka kwa nabii wa mwisho, hajaweza kutumia hata 30% ya aliyopewa hivyo hana sababu ya kwenda kutizama match.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyojifunza mengi kutoka kwa nabii wa mwisho, hajaweza kutumia hata 30% ya aliyopewa hivyo hana sababu ya kwenda kutizama match.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nyie ndio mmeanza kufuatilia mpira juzi 😎.so mnafuata mkumbo tu kwa wengine...angalia style ya uchezaji/kukokota mpira wa Messi na Diego, na style ya gaucho wako aliemuiga Zinedine zidane...in short jamaa yako amekopi from zizo, pamoja na hayo yote and still hajafikia level yake mpaka anastaafu soka, Ustazi kautendea haki mpira ukilinganisha na huyo anaetikisa kiuno kama mtoto wa kike na kuendekeza umalaya jambo ambalo Mungu hapendi, kwa akili yako huyu jamaa utamcompare na akina Diego na Messi kweli!!!...Please give me the statistics za gaucho katika ligi 3 alizocheza then compare na Messi aliecheza only one club! Naomba uniletee now!!

Kitu kingine kijana wangu, usiangalie jina, au vyenga...angalia alichofanya uwanjani je ameleta mafanikio gani katika timu zake? Messi na Maradona ni vipaji kutoka kwa Mungu aliyewaumba na wameutendea mpira ipasavyo kama ni chenga tu na kuuchezea mpira wautakavyo hakuna anaewafikia huo ndio ukweli halisi kijana wangu...mijitu inawapita mabeki wa5 mpaka 6 na wanascore utawalinganisha na gaucho!!! Messi ana uefa 4, 10 La liga tittles and 6 Ballon d'Ore utamlinganisha na gaucho!!

Kuhusu unabii, hilo unalitambua wewe tu... kwa sisi tunaoamini uwepo wa Mungu na mitume wake hatulitambui hilo kijana...hata Maradona na Messi wanaitwa Mungu wa soka lakini sitaki kuamini wala kulitambua hilo...Mungu ninaemjua mimi ni Mungu alietuumba hakuzaa wala hakuzaliwa, ambae, na Mitume wake watabakia kuwa Mitume...
 
Mafanikio makubwa kuliko yote katika mpira ni World Cup, tukumbushe Messi kaisaidia Argentina kuchukua world cup mara ngapi, hoja ya kukopi uchezaji haina mantiki, Messi kajaribu kukopy baadhi ya vitu kwa Maradona , Dinyo ni complete package ni wengine wanapaswa kukopi kutoka kwake. Zinadane naye ni overrated (pengine unamshabikia kutokana na kuamini vitu vinavyofanana), ila wala hana skills za Okocha. Mambo ya umalaya siyo hoja, tunaangalia kinachotokea uwanjani, unamdis Dinyo ni malaya ila unamkumbatia Maradona na madawa yake ya kulevya, vitu vyote hutoka kwa Mungu, hivyo ukisema hiki au kile kimetoka kwa Mungu hutaeleweka unataka kusema nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe acha kuchanganya mautani ya mpira na vitu halisia. Acha kupotosha na usidhani watu wakisema kwa mfano Ronaldo de Lima ni mungu wa mpira wana maana ya Mwenye enzi Mungu muumba mbingu na nchi, si kweli. Kama hilo hujui kaa kando acha watu wafanye ushabiki kwa kadri wanavyoona.

Lakini pia ni mapenzi ya kila mtu kumuona mchezaji fulani ni bora kuliko yule na vile vile hata kufuata mkumbo inakubalika kwa sababu ni issue za ushabiki, hakuna kipimo rasmi. Kuchukua makombe bado haiwezi kuwa sababu kwa sababu hiyo ni kazi ya timu nzima. Tuzo binafsi zinaweza kuwa kigezo ingawaje si kihivyo, issue za kibiashara zinabeba baadhi ya wachezaji bila kusahau upendeleo unaoweza kufanywa na mahirikisho husika.

Kwa hivyo acha mambo ya kutumia umri kwenye kujua nani ni bora kuliko huyu ingawaje una faida ya kuona mengi kuliko wadogo. Kwangu mimi mchezaji bora kwa muda wangu wa ushabiki ni Paul Gazza.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kuhusu Paul Gazza . Alikuwa balaa .
Mimi ni shabiki wa Real Madrid na Arsenal ila ngoja nitaje wachezaji wangu wachache bora bila kujali mafanikio kisoka hapa naongelea kipaji asilia .

1 .Pele
2 . Jayjay Okocha
3 . Mess
4 . Zidane
5 . Paul Gazza
6 .Ronaldo de Lima
7 . Requelme
8 .Alesandro Delpiello
9 . Roberto Carlos
10 .Iniesta
11 .Ronadinho de Souza
12 . Emmanuel Okwi
13 .Edibil Lunyamila
14 .Hussein Amani Masha
15 . George Magere Masatu
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Muombe aje atoe mahari kwenu akuoe. Uwe mke wa pili.
 

Mafanikio huwa yanapimwa katika club na sio national team kijana wangu "Individual club level" hata hili hulijui!! The Top Executive Coaches in the World wakiulizwa nani wanaemkubali utawasikia MESSI MESSI MESSI..wewe kama nani ubishe! Wabongo ndio maana mnafeli sana...ingia Quotes zao uone wakimtaja Messi moja ya mchezaji bora kuwahi kutokea...ila sijasikia wakimtaja gaucho ni ninyi tu wabongo mnaoshinda hukoo vibandaumiza mnadanganyana tu...

Since his first match for Barcelona in 2004, Lionel Messi has won a whopping 30 trophies with Barcelona. But that's just for Barcelona. He's also won an Olympic gold medal with Argentina at Beijing 2008 and he also won the under-20 World Cup.Nov 10, 2019

Messi is not only one of the best players in the world, but apparently he is the best dribbler in the world.

Mimi nabishana kisoka zaidi, na sio kishabiki kijana...nimekuomba facts za jamaa yako in the three leagues he has ever played unajiuma-uma tu...umeishiwa hoja! Kwaheri!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…