WANA JF!
Hapa nchini Finland mjini Helsinki yapo maonesho ya kimataifa ya kutangaza utalii. Karibu nchi zote duniani zimeleta wawakilishi wa kutangaza vivutio vyao hapa ikiwa ni pamoja na jirani zetu wa Kenya.
Cha kushangaza kama kawaida ya Watanzania, jamaa waliotumwa kuiwakilisha nchi yetu katika maonesho haya ya siku saba, walikuwa kwenye banda lao kwa siku moja na nusu tu. Baada ya hapo jamaa wamepanda boti na ninavyo tuma taarifa hii wapo nchini Sweden watumbua kwa raha zao. Cha ajabu Rais wa nchi ya Finland amepita kuangalia na kujionea shughuli katika maonesho haya na alipo fika banda la Tanzania alishangaa kuona analazimika kujiokotea mwenyewe vipeperushi bila kuona wataalam wa utalii Tanzania ili kupata maelezo ya kina kuhusu vivutio vyetu. Vile vile watu wengi hapa wameonyesha nia ya kutembelea Tanzania kwani walikuwa wamejazana kwenye banda na kushangaa kuona halia watu wa kuwapa maelezo.
Wana jamvi hii imekaa je??????