Unapozungumzia watangazaji bora wa michezo hivi sasa nchini hutaacha hata kidogo kulitaja jina la Shafii Dauda wa clouds fm.
Ni mtangazaji makini, ametulia, yuko composed and he knows all there is to know about michezo.
Hana mimbwembwe ya ajabu ajabu na ana uelewa mpana wa mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa hata katika kada zingine.
Ana brain nzuri, hana papara na ni sensible analyst kwa kweli. Naomba tu a solve mambo yake na mamlaka husika ili aendelee kupiga mzigo. Inshallah.
Mwingine kichwa ni Alex Luambano. Ni mweledi sana na anafanya kazi yake kwa umakini mkubwa. Si mtu wa kukurupuka kama baadhi ya watangazaji. Ana uelewa wa mambo mengi pia sio kama watangazaji wengine ukiwauliza Brexit ni nini utasikia_ mimi mtangazaji wa michezo! Alex nae ni moja ya watangazaji makini kabisa hapa nchini kwa sasa.
Issa Maeda ana uelewa mpana pia na yuko professionally fit. Anajua sana ku interact na wenzake. Hawa wanafanya kipindi cha sports extra ya clouds fm kiwe worthy kukisikiza.
Mtangazaji mwingine mzuri na bora sana wa michezo ni yule wanamwita 'ticha' ( somebody Kinja nadhani) wa EAST AFRICAN RADIO. Ana brain kali sana. Aaaah... He is such a professional dude....
Ni mtaalamu, yuko makini na siku zote anafafanua mambo logically. Unajua utalaamu wa michezo sio kumjua Messi au Ronaldo tu. Ni pamoja na uelewa mpana wa dunia kihistoria, jiografia, siasa, utamaduni na hata uchumi.
Watangazaji vijana learn from this guy. Mtapata madini kedekede lakini mkijifanya wajuaji saana mtaishia kuwa half baked presenters for good!
Watangazaji wengine weledi bila wasiwasi ni pamoja na mkongwe Sued Mwinyi wa tbc, Salum Msabaha_ dogo wa Radio one, Ambangile _dogo wa Magic fm ( huyu nae ni mtaalamu sana), Omar Katanga na Oscar Oscar wa EFM pamoja na kaka yao Maestro ambaye ni mtaalamu kweli lakini nafikiri anaremba mno.
Watangazaji wa michezo wababaishaji na wenye mbwembwe za kitoto ni pamoja na Masare wa Radio one na 'mentor' wake Maulid Kitenge wa EFM. Too much unnecessary ego@ kubana sauti.
Wababaishaji wengine ni Enock Bwigane na Jesse John wa tbc pamoja na dada yao Jane John.
Kilumanga wa Magic fm nae ni bonge la kilaza. The way anachambua mambo hata hayo ya michezo tu, unajua kabisa huyu hamna kitu.
Ni kanjanja fulani hivi. Hapo hujamleta kwenye jiografia. Hachelewi kukwambia Venezuela imepakana na Morocco kwa upande wa kaskazini!!