Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,480
- 4,775
Wewe ndio mfuatiliaji wa Matangazo ya mpira.
Sio huyo mpayukaji aliyeanzisha thread.
Mpira bila Charles Hillary na Marehemu Omari Jongo haukusikilizika sheikh kwa watu wenye utimamu kichwani.
Wakati huo fundi mitambo kwenye caravan alikuwa Obi Mwambungu
Msimamizi wa matangazo Nadhir Mayoka
Tukirudishwa studio tunapokelewa na Bujaga Izengo Kadago...
puumbav hakuna swedi mwinyi wala sijui maulid kitenge
Wewe ndio mfuatiliaji wa Matangazo ya mpira.
Sio huyo mpayukaji aliyeanzisha thread.
Mpira bila Charles Hillary na Marehemu Omari Jongo haukusikilizika sheikh kwa watu wenye utimamu kichwani.
Wakati huo fundi mitambo kwenye caravan alikuwa Obi Mwambungu
Msimamizi wa matangazo Nadhir Mayoka
Tukirudishwa studio tunapokelewa na Bujaga Izengo Kadago...
puumbav hakuna swedi mwinyi wala sijui maulid kitenge
Mimi 10 bora wangu ni hawa:
1.Mshindo Mkeyenge
2.Omary Jongo
3.Dominick Chilambo
4.Charles Martin Hilary
5.Barthlomeo Komba
6.Ahmed Jongo
7.Salim Mbonde
8.Abdallah Idrisa Majura
9.Mikidad Mahmoud 'Brother Mick" na
10.Abdul Ngarawa
Nimesikitika kutowaona wafuatao:
1. Ahmed Kipozi; huyu alikuwa nanifurahisha sana kwa pozi zake.
2. Salim Seif Nkamba
Honestly mi sijawahi sikia mtangazaji akiitwa Salim Seif Nkamba
Safi sana Chomba '..Orodha na ushahidi kama huu'
Lengo la thread ni kuwaamsha watangazaji wa mpira kuboresha mbinu zao za utangazaji kwa ajili ya jamii.
Nitaomba mwongozo wa msimamizi wa forum hii namna anavyoweza kunisaidia kumpa zawadi Mtangazaji au mwakilishi wake atakayekuwa ametajwa zaidi ya wengine kupitia JF.
Charles Hillary, Omar Jongo, the late Dominic Chillambo(huyu aliweza kutangaza mara kadhaa dk.90 mwenyewe)
...Mikidadi Mahmood hakuwahi kuwa mtangazaji mzuri wa mpira RTD wakati huo alijaribu lakini hakuwa na mvuto. Hii pia ilikuwa kwa Julius Nyaisanga alijaribu kutangaza mechi kati ya Simba Vs Coastal Union uwanja wa Taifa mwaka 89 lakini hakurudi tena. Lakini ninaowakumbuka ni Charles Hilary (mwanzilishi wa neno majalo akimaanisha cross na darizi mchezaji akipigwa kanzu na sauti yake husikika pia kwenye kiashirio cha kuanza kwa kipindi cha Sports Leo Radio One ile ilikuwa mechi ya Simba Vs Sports Club Villa ya Uganda 1990 goli lilofungwa na aliyekuwa kocha mchezaji wa Simba Hassan Hafif) , Ahmed Jongo (aliyeanzisha msemo wa maguu 12 ya mtu mzima kunapokuwa na kupigwa penati), Salim Mbonde (Kumbuka Mechi ya Simba Vs National Al- Ahari 1984) , Dominick Chilambo (aliyeibatiza timu ya Pamba ya Mwanza wakati ule jina la TP Lindada), baadaye wakaja akina Sued bin Mwinyi,Halima Mchuka,Jesse John,sasa wamo pia akina Maulid Kitenge na Issac Gamba (Radio One), Tom Chilala (RFA) na wengineoumesahau, mikidad mahmood and nadhir mayoka. Ilinoda wakiwamo uwanjani Zamoyoni mogella, juma mkambi, makumbi juma, abeid mziba