Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,547
- 7,167
Ukitukia angalau inaonekana kama unatamani ingelikuwa zaidi ya hapoSasa hilo Angalau linamakosa gani?
Kiswahili hakikuwi?
Hapo angalau umedadavua kidogoUkitukia angalau inaonekana kama unatamani ingelikuwa zaidi ya hapo
Angalau lina maana ya at least lakini ni katika muktadha fulani tu, nyingine haifai
Mfano unaweza kusema
"Kila mfanyakazi awe analipwa angalau sh.laki moja kwa mwezi." Hapo ni sawa
Ila ukisema "Angalau watu 10 wamefariki kwa kipindupindu". Inaleta ukakasi
Ingetakiwa " Watu wasiopungua 10 wamefariki kwa kipindupindu"
Kiswahili kinatupiga chengaAt least humaanisha kadirio..
Hivyo ikisemwa INAKADIRIWA.... italeta maana.
Neno angalau humaanisha afadhali, ahueni and so of likes
Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa huoni takriban ndiyo sahihiNeno 'Angalau' halina makosa yoyote. Neno hilo ni tafsiri ya moja kwa moja ya neno la Kiingereza, 'At least'.
Neno 'Takriban' ama 'Takribani' kwa lugha ya Kiingereza ni 'Approximate' na si At least. Neno 'Takriban' lina maana ya idadi inayokaribiana na idadi kamili (idadi ya makadirio).
Neno "Takribani' laweza kutumika kama 'mbadala' lakini haimaanishi kuwa neno hilo ndilo sahihi.Sasa huoni takriban ndiyo sahihi
Bado sijakubaliana na weweNeno "Takribani' laweza kutumika kama 'mbadala' lakini haimaanishi kuwa neno hilo ndilo sahihi.
Kuna utofauti hapo, nadhani umekwisha kuuona.