Watangazaji wa lugha ya Kiswahili DStv Kombe la Dunia mnaboa sana

Watangazaji wa lugha ya Kiswahili DStv Kombe la Dunia mnaboa sana

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
10,198
Reaction score
35,323
Kusema ukweli utangazaji wa mpira Kombe la Dunia kupitia DStv lugha ya Kiswahili hauvutii.

Hao watangazaji ni kama siyo wataalam kwa hiyo kazi, maneno mengi, stori nyingi zisizoendana na matukio uwanjani, kalele nyingi mpaka mnasahau kama mnatangaza mpira, hamna taarifa na takwimu za wachezaji, mkimjua moja mtamtaja huyu mpaka mpira uishe loh!

Kwanini msijifunze kutoka kwa wale watangazaji kwenye lugha ya Kingereza? Wametulia katika utangazaji wao na wanaongea vitu muhimu tu.

Wakati mwingine mnajifanya kama wachambuzi au makocha wa timu husika, mnaboa kwa kweli.
 
Kwani lazima kuwackiliza?
Ndo tumewekewa hao waswahili bila kuomba ukiweka 223 utawakuta tu, wanadhani kila mtu anahitaji kalele ili kuchangamka wakati wakufunga gooooooool.....
 
Hii ni kweli. Nakumbuka game ya kwanza world cup kuna muda walikua wanamuongelea mbappe na wachezaji wengine wa France wakati bado game inaendelea...
Ni kweli mkuu angalau huyu Charles hilaly wa kipindi anatangaza kwenye chanel ya azam anaweza hana kelele nyingi na anatangaza matukio tu.
 
Ahahahha kuna hawa wa TBC nao wanakelele vibaya mno, wakichafukwa wataisifia timu mpaka ukasirike.
 
Back
Top Bottom