Watangazaji wa michezo vichwa, ovyo

Watangazaji wa michezo vichwa, ovyo

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,203
Unapozungumzia watangazaji bora wa michezo hivi sasa nchini hutaacha hata kidogo kulitaja jina la Shafii Dauda wa clouds fm.

Ni mtangazaji makini, ametulia, yuko composed and he knows all there is to know about michezo.

Hana mimbwembwe ya ajabu ajabu na ana uelewa mpana wa mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa hata katika kada zingine.

Ana brain nzuri, hana papara na ni sensible analyst kwa kweli.

Mwingine kichwa ni Alex Luambano. Ni mweledi sana na anafanya kazi yake kwa umakini mkubwa.

Si mtu wa kukurupuka kama baadhi ya watangazaji. Ana uelewa wa mambo mengi pia sio kama watangazaji wengine ukiwauliza Brexit ni nini utasikia_ mimi mtangazaji wa michezo! Alex nae ni moja ya watangazaji makini kabisa hapa nchini kwa sasa.

Issa Maeda ana uelewa mpana pia na yuko professionally fit. Anajua sana ku interact na wenzake. Hawa wanafanya kipindi cha sports extra ya clouds fm kiwe worthy kukisikiza.

Mtangazaji mwingine mzuri na bora sana wa michezo ni yule wanamwita 'ticha' ( somebody Kinja nadhani) wa EAST AFRICAN RADIO. Ana brain kali sana. Aaaah... He is such a professional dude....

Ni mtaalamu, yuko makini na siku zote anafafanua mambo logically. Unajua utalaamu wa michezo sio kumjua Messi au Ronaldo tu. Ni pamoja na uelewa mpana wa dunia kihistoria, jiografia, siasa, utamaduni na hata uchumi.

Watangazaji vijana learn from this guy. Mtapata madini kedekede lakini mkijifanya wajuaji saana mtaishia kuwa half baked presenters for good!

Watangazaji wengine weledi bila wasiwasi ni pamoja na mkongwe Sued Mwinyi wa tbc, Salum Msabaha_ dogo wa Radio one, Ambangile George_dogo wa Magic fm ( huyu nae ni mtaalamu sana), Omar Katanga wa Azam na Oscar Oscar wa EFM pamoja na kaka yao Maestro ambaye ni mtaalamu kweli lakini nafikiri anaremba mno.

Watangazaji wa michezo wababaishaji na wenye mbwembwe za kitoto ni pamoja na Masare wa Radio one na 'mentor' wake Maulid Kitenge wa EFM. Too much unnecessary ego@ kubana sauti.

Wababaishaji wengine ni Enock Bwigane na Jesse John wa tbc pamoja na dada yao Jane John.

Wale wa sibuka fm nao ni washambashamba fulani hivi. Too much ubabaishaji.
Tom Chilala naye anaharibu sana anaporeemba sauti.
Kilumanga wa Magic fm nae ni bonge la kilaza. The way anachambua mambo hata hayo ya michezo tu, unajua kabisa huyu hamna kitu.
Ni kanjanja fulani hivi. Hapo hujamleta kwenye jiografia. Hachelewi kukwambia Venezuela imepakana na Morocco kwa upande wa kaskazini!! Au Monaco iko karibu na Canada!
 
Umemsahau Jeff leya yupo smart sana,na kuna jamaa anaitwa James jonh wa ebony fm huwezi juta kuwasikiliza,ila hawa wakina kitenge ni kelele tu
 
Huyu ni Mchambuzi si mtangazaji.
Ni kwenye uchambuzi ni zero
 
Ulipomtaja tu Maulid Kitenge ' fasta ' sana nikamkumbuka ' Mwarabu ' mmoja hivi Merey Balbhabou Mzee wa TIOT. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Shaffih Dauda Hanna kitu Mkuu nafikiri umekurupuka
bora hata ungemtaja Edger Kibwana jamaa anajua sana pamoja na mwalimu Tigana
 
Ila Kitengo pamoja mapungufu yake anajua kuhoji na kukichangamsha kipindi!
 
mzee baba mtoa hoja hili analichanganya sana..nadhani naye haujui mpira vizuri...


kuna watangazaji wa mpira na wachambuzi wa mpira.

shaffih si mtangazaji ni mchambuzi
kitenge si mchambuzi ni mtangazaji
jeff lea si mtangazaji ni mchambuzi

hawa watu hutofautiana sana, leo ukimweka shaffih atangaze kipindi cha mpira sidhani kama atafit lakini ukimweka kwenye uchambuzi atafit sana...Mchambuzi huwa anakuwa na uelewa mkubwa kuhusu mpira lakini pia anakuwa anajua sana historia ya mpira sometimes anaweza kutabiri. Kinyume chake ni mtangazaji.


kidogo nitakuwa nimeelewesha hapo.
Kuna Tofaut kubwa Kati Ya Wachambuzi wa Mpira na Watangazaji Wa Michezo...Dont confuse them
 
Mkuu funguka japo kidogo

Ukishaona naandika hilo neno la naomba niishie hapa tafadhali halafu hadi naliwekea rangi Nyekundu jua ni Nyeti mno na limekaa Kimaadili sana ila wenye akili wameshajua nimemaanisha nini na hasa hasa Watu wa Mpira hasa wa Bongo na mambo ya ' Waarabu ' bila kusahau wanaoijua historia ya huyo Mtangazaji tokea alipokuwa INDEPENDENT PUA PUA MEDIA Mikocheni Industrial Area .

Kila la kheri.
 
Dah..kuna mmoja huwa anajichanganya...anatohoa lugha... kipindi kizima yeye anakomaa na neno "kupata matokeo"....sijui mechi gani huwa inaisha bila kupata matokeo...[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mkuu hapo kwa Shafii umeingia chaka. Labda kama amekutuma umpe kiki. Hakuna mchambuzi ambaye yupo biased kama Shafii.

Siku zote ili uwe mchambuzi wa kuheshimika lazima kwanza uweke unazi pembeni. Uende na facts, bila kujali ukweli unakuuma kiasi gani. Shafii hanaga hili huwa anaonyesha ushabiki wa wazi kwa Man United
 
Kampista Tigana Ticha Maestro Kitenge nawakubali sana hao ni kwenye michezo.
 
Back
Top Bottom