kasyabone tall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2009
- 254
- 63
Kitu kinachonikera kwa tv zetu zote hasa wa startv na TBC ni pale wanapoacha kazi yao na kujiingiza kupiga kampeni. Wanaeleza hisia juu ya chama fulani kuliko kufanya kazi ya kuripoti kile kinachotokea. Utasikia mtangazaji anatangaza chama cha CCM kimenitoa mbali, hii ni kauli ya ushabiki juu ya chama, Kitu amabacho kinaonyesha huyu mtangazaji hawezi kuripoti vizuri kwa chama cha upinzani kama Chadema ambacho hakija mtoa mbali. Lakini kinachochangia yote haya ni ukosefu wa elimu kwa watangazaji wetu. Nafikiri sasa ni wakati mzuri wa vyombo vya habari kutungiwa sheria juu ya kuripoti habari za uchaguzi, Kama sivyo vyama vya upinzani vitashindiwa kwenye vyombo vya habari.