Watangazaji wa vipindi vya Michezo wanakera sana kuwahoji watu wasio sahihi juu ya mambo yanayozihusu Yanga na Simba

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Habari wanaJF,Binafsi nilikuwa msikilizaji mzuri wa vipindi vya michezo ktk Redio zetu za Tz, hasa E-FM,Magic FM,RFA,Clouds na zingine kadhaa,lakini nilichoshwa na Radio hizi kuwa zinatafuta taarifa kwa watu ambao kwa mtazamo wangu si watu sahihi.Mimi sina taaluma ya uandishi wa habari lakini ktk mtazamo wa kawaida tu ambao hauhitaji taaluma hiyo,niligundua kabisa kuwa kuna mapungufu makubwa ktk utafutaji wa taarifa.

Yanga na Simba kwa siku za karibuni wamekuwa katika kipindi ambacho wao wanakiita mabadiriko ya mifumo ya uendeshaji wa timu zao na Simba wao wamefika mbali kiasi ukilinganisha na watani wao.Dukuduku langu ni pale wanapokuwa wanampigia Simu Bi Hindu au Mzee Akilimali kutaka kupata maoni yao wakati hawana utaalamu wowote ule ktk mambo ya Hisa na soka kwa ujumla,wapo mashabiki wengi na wanachama wenye uwezo wa kutoa maoni mazuri zaidi.Badilikeni Jamani
 
Mzee akilimali anawaambia wana yanga kuwa yanga haihitaji sana pesa...,bali hekima yake inatosha kabisa kuiongoza yanga na ikafanya poa ndani hadi nje ya nchi hhhhhhhh.....,nahizi mvua,naona kambale wamezaliana mara dufu..,ngoja nikachukue ndoano yangu nikapate kitoweo cha Bure...
 
Mpira wa sasa ni pesa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…