SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,265
Ninasikiliza radio na kutazama sana tv. Watangazaji wengi wa tv na radio wanatumia lugha kwa namna ambayo
inanipa mashaka kwamba kwenye vyuo vya uandishi habari hakuna somo la lugha kiswahili/ kiingereza/kifaransa.
Nionavyo mimi ingawa kifaransa sio lugha itumikayo hapa nchini tz, ni vizuri misingi yake ya matamshi ikafundishwa
kwenye vyuo vya uandishi wa habari. Nilimsikia mtangazaji mmoja wa tv ninayoitazama mara kwa mara akitangaza
habari zilizomhusu rais wa France. Alitamka jina la rais wa ufaransa hivi:frankois hollande.Niligundua mara moja kwamba
mtangazaji huyo hajui/hajafundishwa kanuni za kutamka maneno ya kifaransa. Natoa wito kwa vyuo vya uandishi
wa habari kufundisha vizuri hii lugha.
Tuje kwenye kiswahili. Hapa namlaumu sana mtangazaji mmoja wa Star Tv ambaye hutumia neno 'kuweza' vibaya sana. Jana nilimsikia akisema: "Watu 71 waliweza kufariki baada ya meli kuzama huko karibu na kisiwa. cha Chumbe" Kwenye michezo utamsikia: "Timu A iliweza kufungwa mabao 2 kwa 1 na timu B"
Mimi sikubaliani na matumizi ya neno 'kuweza' kwenye hizo sentenso! Kwenye redio moja nilisikia " Wasichana mkoani Mara wanaandaliwa kukeketwa sehemu za siri" Pia nilisikia: " Mwanamke mmoja alibakwa kwa nguvu" Nauliza:Kukeketwa sehemu za siri maana yake nini? Au kubaka kwa nguvu ndio nini?
Kwenye kiingereza ndio kabisaaaa! Neno 'pharmacy' utasikia linatamkwa famas yaani utafikiri hii lugha haifundishwi hapa nchini. Jamani watangazaji na wanahabari,
jitahidini kunyoosha lugha mnazotumia kutangaza!