Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Yaani kuna kitu kinanikera mno kuangalia stesheni nyingi za TV Tanzania. Ni kwamba watangazaji wengi sana wa TV, wanawake kwa wanaume, wanapofanya matangazo wanakuwa wamengangamala utafikiri wanaishi kwa kula cement. Unakuta mwili umejikaza hawako natural kabisa, wako very conscious kwamba wanaangaliwa.
Halafu kitu kingine kinaniudhi sana ni karibu Watangazaji 95% wa TV na Radio Tanzania wanabadilisha sauti zao. Na wengi wanaongea kwa kusita sita (kwa pause) wakifikiri ndio inapendezesha kutangaza. Kwa nini lakini? Kwa mfano kuna dada mmoja anatabiri hali ya hewa TVT huwa nikimwona tu nabadilisha channel, ananiudhi mno kujibadilisha sauti na kujifanya anaongea kwa pause.
Kuna wakati Mtangazaji nguli Tanzania, Charles Hilary, alisema wanaongea "kizunguzungu" dada mmoja alipozidisha mno kuongea kwa pause. Charles alimuuliza kama alikuwa ameishi nje ya Tanzania muda mrefu kutokana na lafidhi yake, na huyu dada akasema hapana, ni mazoezi tu. Ndipo Charles akashangaa kwamba ni mazoezi ya kuongea kizunguzungu?
Kwa nini msiwe natural katika kukaa na kuongea? Hivi hakuna mafunzo mnapewa? KUna wengine wanadhani wakiongelea puani ndio Kiswahili chao kinaonekana cha kisomi, ovyo kabisa. Nani aliwaambia kubadili sauti zenu hizo na kuongea kwa pause kunapendezesha utangazaji? Mnakera mno na mnaharibu lafidhi ya Kiswahili. Acheni ulimbukeni. Hamuoni CNN, BBC Skynews wanavyoongea? U-artificial wa nini kwenye sauti zenu? Nani aliwaambia mkiongea naturally hampendezeshi matangazo?