Kweli,sema zebwela bado kabaki kwenye misingi yake.Huyo huyo Kitenge. Kaona usomaji wa magazeti lazima ufoke na kelele za kujirudiarudia kama anaongea na viziwi.
Zembwela akiwa EA Radio alikuwa anafanya kazi kwa utulivu sana hata David Rwenyagira ila combination yao na Kitenge watakuja kutoka studio taya zimetanuka.
Wale jamaa walikuwa wanajua sana kazi wakiwa pamoja walikuwa wanafanya nasikiliza kipindi chao kila muda.Kweli ila bado zebwela kabaki jwenye misingi yake.
Ila kuna combination huwa zinaendana. Kama ya Dav, makee na Ian nilikuwa naenyoy "Ndinga mpya town " daily but now.......... Sina mood kabisa
Sent using myLG leon
umeongea kwa sauti sanaaMiiiiimiiii niii Jojiiiiiiii mvaaaviatuuu wa aiiitiiiiiviiiiii
Pumbavu weweWewe utakuwa una dada yako anaongea hivyo na unadhani ni ujiko wa kupata shemeji mwenye gari uwe unaendesha
Wachungaji sio watangazaji ni emotions za mahubiriHujawasikia wachungaji wewe
😀 😀 😀 😀 😀Nimetoka kusikiliza habari kwa bahati mbaya kutoka Morning Star Radio ama hakika wewe mtangazaji uliyesoma habari leo Tarehe 14.04.2020 saa 20:00 ni tatizo kubwa sana.
Nani ana mawasiliano na kiongozi yeyote wa Morning Star Media?
fala sana mkuu😂😂😂😂😂Mimi ni hemedi kivuyoo....hahaahaha asee
Mimi ni jooooooooji maratuuu wa itviiiiiiiii maraaaaaaam
Halafu nao hujifanya wanamaisha Fulani kumbe wagangaji tu.Wanaigana sana mfano redio za FM staili ilibuniwa na clouds hawajawahi iboresha.Wengi wao elimu in ndogo ila ni wajuaji sana.Wanaigiza mpaka maisha, kuvaa mawigi na kujichubua kwa wanawake,uzuri wa bandiabandia na upotoshaji wa maadili wanaongoza.Yaani kuna kitu kinanikera mno kuangalia stesheni nyingi za TV Tanzania. Ni kwamba watangazaji wengi sana wa TV, wanawake kwa wanaume, wanapofanya matangazo wanakuwa wamengangamala utafikiri wanaishi kwa kula cement. Unakuta mwili umejikaza hawako natural kabisa, wako very conscious kwamba wanaangaliwa.
Halafu kitu kingine kinaniudhi sana ni karibu Watangazaji 95% wa TV na Radio Tanzania wanabadilisha sauti zao. Na wengi wanaongea kwa kusita sita (kwa pause) wakifikiri ndio inapendezesha kutangaza. Kwa nini lakini? Kwa mfano kuna dada mmoja anatabiri hali ya hewa TVT huwa nikimwona tu nabadilisha channel, ananiudhi mno kujibadilisha sauti na kujifanya anaongea kwa pause.
Kuna wakati Mtangazaji nguli Tanzania, Charles Hilary, alisema wanaongea "kizunguzungu" dada mmoja alipozidisha mno kuongea kwa pause. Charles alimuuliza kama alikuwa ameishi nje ya Tanzania muda mrefu kutokana na lafidhi yake, na huyu dada akasema hapana, ni mazoezi tu. Ndipo Charles akashangaa kwamba ni mazoezi ya kuongea kizunguzungu?
Kwa nini msiwe natural katika kukaa na kuongea? Hivi hakuna mafunzo mnapewa? KUna wengine wanadhani wakiongelea puani ndio Kiswahili chao kinaonekana cha kisomi, ovyo kabisa. Nani aliwaambia kubadili sauti zenu hizo na kuongea kwa pause kunapendezesha utangazaji? Mnakera mno na mnaharibu lafidhi ya Kiswahili. Acheni ulimbukeni. Hamuoni CNN, BBC Skynews wanavyoongea? U-artificial wa nini kwenye sauti zenu? Nani aliwaambia mkiongea naturally hampendezeshi matangazo?
Mauridi wa kitenge naye yupo poa sana.Jacob tesha na Masoud Masoud hao Jamaa Mimi ndio ninawakubali sana
Mkuu umeongea point sana. Kuna mahojiano wanafanya waandishi wanaongea mambo na kuuliza maswali ya kitoto na kijinga sana utafikiri waliishia darasa la nne!Halafu wengi ni weupe kichwani hawana exposure..wakiwa wanajadili kitu unaona kabisa hawana wanachokijua,ni ile tu kwamba wabongo wengi tunapenda vitu rahisi rahisi.. hatupendi kuumiza kichwa.
Mkuu nilifikiri mie ndio nina tatizo kutopenda mijadala, kumbe ni ukihiyo wa hawa waandishi wa habari ambao uko wazi kwa watu wengi!Wengi hawawezi kuendesha mjadala angalau wa dakika kumi!
Hawafanyi utafiti wala hawajui wanachokifanya!
Ndivyo walivyo hawa watanganyika! Wanapenda hadithi za ngono tu, kunyoa viduku na kubeti!
Ukiwapa mjadala wote wanakimbia! Akijitahidi ni dakika mbili anaanza kubabaika!
Sent using Jamii Forums mobile app
Wamefanya sauti kuwa mtindo! Halafu sauti fake, artificial za kujipa! Wapumbavu sana hawa. Nani anapenda masauti yao feki yanaharibu kiswahili chetu?Kitenge anatumia nguvu sana.
Na kuna wale watangazaji wa vipindi vya bongfleva sauti zao wote kutoka radio tofaut hufanana.
Wee acha tu....Lini ulimtembelea Christine Amanpour nyumbani?
Thread inasema watangazaji wengi wanatumia sauti fake na sio prefessional, tatizo ni nini sasa? Kama wewe ni mmoja wa hao wachache ambao hamtumii sauti bandia hongera sana. Waambie wenzako kuweka sauti fake kunakera wasikilizaji au watazamajihapa bongo kila kitu kinaonekana sicho hata kama shida ipo kwa wachache
Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ndio maana huwa siwasikilizi.Wamefanya sauti kuwa mtindo! Halafu sauti fake, artificial za kujipa! Wapumbavu sana hawa. Nani anapenda masauti yao feki yanaharibu kiswahili chetu?