Jamani mimi nauliza,nauliza kwa sababu sielewi mwenzenu,yaani sielewi kabisaaaaaaa.Hivi kwa nini tunanyamaza kimya huku maadili ya jamii yetu yanazidi kuharibiwa na watu wachache,tena wageni wenye ajenda zao za ziri?Hivi kwa nini lakini.Jamani tumepigwa ganzi na nani? Hivi tumekubali kabisa watoto wetu wafolenishwe hadharani na vichupi kwa visingizio vya biashara.Biashara gani hizi uchwara ambazo lazima watu watembee uchi ndio zifanyike.Jamani hivi tumekubali kabisa matendo yanayoashiria ngono yaonyeshwe hadharani kabisa kwenye haya wanayoita makongamano.Hatuoni kwamba huku ni kuhamasisha ngono na kutudhalilisha?Jamani unapiga vita ukimwi huku unahamasisha ngono,ni ujinga gani huu!Watanzania wenzangu nani ametulaza usingizi mnene kiasi hiki?Mbona hatunyanyuki na kukemea ujinga huu na kusema sasa basi.Wazazi mko wapi?Mmekubali watoto wenu wafanywe mataahira mbele yenu kabisa, lakini mkoje?Mbona hamuamki mkaihoji na kuiwajibisha serikali katika hili.Poleni sana ndugu zangu,mtakapo zinduka mtakuwa mmechelewa sana, wenzenu watakuwa wameshamaliza kazi.Amkeni basi katika usingizi wenu mnene mkaliepushe taifa hili na maangamizi ya kutisha yanayo linyemelea taifa letu.Watumishi wa maruhani, wanasema kukaa uchi ni mila yetu.Hawa ni watu waliopotoshwa kabisa kimaadili na maruhani.Wamepofushwa fahamu zao wasijue kwamba katika bustani ya Eden baada ya dhambi kuingia,Mungu mwenyewe aliwavalisha Adam na Hawa mavazi.Wanasahau pia kwamba nyakati ambazo watu walikuwa hawavai nguo,Mungu aliziita nyakati za ujinga,na kwamba Mungu anasema alijifanya hazioni!Lakini sasa anataka watu waenende inavyowapasa.Wanasahau pia kwamba sasa Mungu ameamuru watu wote wavae mavazi ya kujisetiri.Wazazi wenzangu,watanzania wenzangu, tusidanganyike na mafundisho ya mashetani ambayo sasa yamesambaa kila mahali kwa nia ya kutupotosha kabisa.Kwa nia mbaya kabisa maruhani na vikaragosi vyao wanatumia kila njia kulipotosha taifa letu.Tusimame imara na kusema hapana na ujinga wao sasa basi.