Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Wafanyabiashara 26 watakaonufaika na Tsh. Bilioni 1.6 za UNDP (Program ya FUNGUO) wapatikana
UNDP kupitia program ya Ubunifu wa Ufunguo (FUNGUO) imeweka wazi kuhusu wanufaika wa awali wa Tsh. Bilioni 1.6 ambazo zinatarajiwa kugaiwa kwa washindi 26.
Biashara 26 za ubunifu zilichaguliwa kati ya biashara 363, zikitokea sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Utalii, Uvuvi, Afya na Elimu, nyingi zikitumia teknolojia katika kujiendesha. Jumla ya waombaji waliojiandikisha kupitia mtandao ni 934.
Zoezi hilo lililoanza Juni 2022 likilenga makampuni yenye mwelekeo wa kufanya mabadiliko chanya na biashara ndogondogo zenye mwelekeo wa kukua zaidi ikiwa pia ni sehemu ya program ya “Mazingira ya Kibiashara, Ukuaji na Ubunifu” yaani BEGIN (Business Environment, Growth and Innovation).
FUNGUO ambayo inafadhiliwa na Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Uingereza na UNDP, inafanya mradi huo kwa kushirikiana na UNCDF na Tume ya Sayansi na Teknolojia COSTECH.
Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa kutoka Umoja wa Ulaya, Hans Stausboll amesema umoja huo unaongeza ufadhili ili kuchangia ukuaji na uwekezaji wa sekta binafsi Nchini Tanzania.
Amesema: “Nafasi ya sekta binafsi hususani vijana inaleta chachu ya maendeleo na mabadiliko ya Tanzania, program ya Ufunguo ni mfano mzuri unaoonesha nia yetu ya dhati katika ajenda hiyo.”
Naye, Eduarda Gray ambaye ni Kaimu kurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Kigeni, Jumuiya ya Madola na Maendeleo, amesema: “FCDO inafuraha kubwa ya kuendeleza mchango wake katika urathi wa Mfuko wa Ubunifu wa Maendeleo ya Watu yaani HDIF (Human Development Innovation Funding) kwa kupitia Program ya kibunifu ya Funguo.
Upande, Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Christine Musisi amegusia jinsi shirika hilo linavyolenga kukuza uwezo wa vijana kupitia njia mbalimbali ikiwemo ufadhili wa kifedha, pia kuweka mazingira wezeshi kwao.