Watanzania 34.3% ni wachawi, hawaamini Mungu, Mtume wala Jah

Takwimu hizi naweza sema ni za uwongo. Ni lini huu utafiti ulifanyika mpaka zikapatikana takwimu hizo? Je hii ni kwa mwaka gani ama umejitungia tu?
 
Dini za jadi (34.3%), Ukristo (33.5%), Uislamu (31.4%), wengineo (0.8%)

Takwimu hizi zinaweza kuwa hazina maana lakini zinatoa taswira ya imani za Watanzania.
Mkuu,bora kuwa mchawi kuliko kuabudi hizi dini za kuletewa na wazungu na warabu,wametuetea dini halafu wanatudharau
 
Soma kichwa cha uzi kinaelezaje?
Acha kupinga ulichoandika mwenyewe.
Kichwa cha uzi umeandika [h=2]" Watanzania 34.3% ni wachawi, hawaamini Mungu, Mtume wala Jah."
Dini za jadi (34.3%), Ukristo (33.5%), Uislamu (31.4%), wengineo (0.8%)[/h]
Takwimu hizi zinaweza kuwa hazina maana lakini zinatoa taswira ya imani za Watanzania.

Unajichanganya sana umesema watanzania 34.3 ni wachawi,hawamwamini Mungu,Mtume wala Jah.
Nikakuuliza kwamba kumtomwamini Mungu,Mtume au Jah ni uchawi?kisha unauliza nisome kichwa cha uzi.
C.C Kiranga
 
Last edited by a moderator:
Hii mada yako ina mahusiano yoyote na hili jukwaa?

Yani kuna watu humu JF mpo muda mrefu ila hadi leo hamjui namna ya kutumia majukwaa.

Inaonekana walimu wako walipata tabu sana katika kukufundisha.

Mods, pelekeni hii jukwaa husika.

Invisible, Cookie
 
Ukiulizwa siasa nini hutajibu, utaishia kusema ni chadema na na ccm.
 
Last edited by a moderator:
Acha kupinga ulichoandika mwenyewe.
Kichwa cha uzi umeandika [h=2]" Watanzania 34.3% ni wachawi, hawaamini Mungu, Mtume wala Jah."

Unajichanganya sana umesema watanzania 34.3 ni wachawi,hawamwamini Mungu,Mtume wala Jah.
Nikakuuliza kwamba kumtomwamini Mungu,Mtume au Jah ni uchawi?kisha unauliza nisome kichwa cha uzi.
C.C Kiranga

Inawezekana kiswahili hukijui,

Niliposema watanzania 34.3% ni wachawi,hawaamini Mungu wala Jah ninamaana pana zaidi, Makundi yote matatu ama manne yapo kwenye hizo asilimia, usiwaweke kwenye jumla ya kuwa wachawi bali hao ni sehemu ya makundi hayo.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo dini za jadi ni uchawi na upuuzi ila za kizungu na kimanga ndiyo za kistaarabu?
Safari tunayo ndefu sana. Je buddhists na hindus ambazo ndiyo zinaongoza kwa wingwa wauminii zinatoa taswira gani kwa waasia?
Dini za jadi (34.3%), Ukristo (33.5%), Uislamu (31.4%), wengineo (0.8%)

Takwimu hizi zinaweza kuwa hazina maana lakini zinatoa taswira ya imani za Watanzania.
 
Inawezekana kiswahili hukijui,

Niliposema watanzania 34.3% ni wachawi,hawaamini Mungu wala Jah ninamaana pana zaidi, Makundi yote matatu ama manne yapo kwenye hizo asilimia, usiwaweke kwenye jumla ya kuwa wachawi bali hao ni sehemu ya makundi hayo.
asilimia zipi hizo 34.3

we ndo hujui kiswahili,ujanja mwingi mbele giza,unapokuwa na maana pana zaidi uwe unaleta ikiwa inaeleweka siyo unafanya iwe na maana pana kwa fikra zako binafsi akilini.
 
Soma kichwa cha uzi kinaelezaje?
Usitake kuwakashifu watanzania kwa sababu hawajaonyesha mwamko wa mageuzi kama ulivyotarajia.
Usipende kuwatusi na kuwadhihaki watu ambao kisiasa labda wanatofautiana na wewe. Tunajua sana unachotaka kusema.
Acha hiyo!!!
 
Nadhani unatangulia kula mboga kabla ya ugali, takwimu ni za Tanzania, sasa wewe unataka nilete takwimu toka wapi ndipo uelewe??
 
Dini za jadi (34.3%), Ukristo (33.5%), Uislamu (31.4%), wengineo (0.8%)

Takwimu hizi zinaweza kuwa hazina maana lakini zinatoa taswira ya imani za Watanzania.

Licha ya kwamba agenda yako hapa ni kufufua hisia za udini kwa ajili ya uchaguzi wa Chalinze, kwa taarifa yako ni kwamba sio lazima kwa kila asiyeamini katika dini za kuletwa ni mchawi, anaweza kuwa ni muumini wa dini za asili. Pia ni vizuri ukatambua kuwa uchawi pia ni imani ambayo ina wafuasi wengi ambao pia ni waumini wa dini zote unazozijua.
 
asilimia zipi hizo 34.3

we ndo hujui kiswahili,ujanja mwingi mbele giza,unapokuwa na maana pana zaidi uwe unaleta ikiwa inaeleweka siyo unafanya iwe na maana pana kwa fikra zako binafsi akilini.

Kuna watu wasipokuelewa maneno na matendo yako, mshukuru Jah, wewe bado unafikra chanya, wakianza kukuelewa jichunguze ni wapi umeanguka maana umeanza kuwaza kama wao
 
Inawezekana kiswahili hukijui,

Niliposema watanzania 34.3% ni wachawi,hawaamini Mungu wala Jah ninamaana pana zaidi, Makundi yote matatu ama manne yapo kwenye hizo asilimia, usiwaweke kwenye jumla ya kuwa wachawi bali hao ni sehemu ya makundi hayo.

Kama ulimaanisha hivyo, kwa nini ume narrow heading na statement yako.
 
Back
Top Bottom